Mkurugenzi wa Taasisi ya Bihimba Foundation Bihimba Mpaya (kulia), mwenye shati la bluu bahari akiwe katika picha ya pamoja na watoto wanaolelewa kwenye kituo cha Msongola Orphanece Trust Fund.
NA ASHA MWAKYONDE, DAR ES SALAAM
MKURUGENZI
wa Taasisi ya Bihimba Foundation ,Bihimba Mpaya anesema kuwa watoto
yatima wanaolelewa katika vituo vya Kulelea watoto hao wanahitaji
faraja ili wajione hawajatenga na jamii.
Akizungumzia
jijini Dar es Salaam juzi wakati akitoa msaada wa vitu mbalimbali
vikiwamo vifaa vya shule katika kitu cha Kulelea watoto yatima cha
Msongola Orphanace Trust Fund kilichopo Kata ya Msongola Wilayani
Temeke Bihimba amesema watoto hao wakitembelewa mara kwa mara wanajihisi
wapo na wazazi wao.
Amesema
kuwa kupitia taasisi hiyo kwa kushirikiana na tMaandao wa 24 technical
Radio& kujoka tv wametoa msaada huo ili kuwawezesha watoto hao 48
wanaolelewa katika kituo hicho nao wajisikie kuwa hawajatenga na jamii
yao.
"Nimeweza tena
kukabidhi, vyakula mbalimbali na vifaa vya shule ili viweze kuwasaidia
watoto hawa kwani hata mimi Sina baba wala mama wazazi wangu
walifariki nikiwa darasa la tatu shule ya msingi kichangachui iliyopo
Kigoma Ujiji nikiwa darasa la tatu,"anesema Bihimba.
Bihimba amevitaja vitu hivyo kuwa ni vifaa vya shule, sukari, nyama, Maharage, sabuni ,mikate na unga wa sembe.
Mkurugenzi
huyo ameongeza kupitia Bihimba Foundation atakuwa anawatembelea watoto
hao mara kwa mara na kuwasaidia misaada mbalimbali wanao hitaji.
Aidha Bihimba amewashauri watoto hao kwamba wasivunjike mioyo kwa kuishi yatima na badala yake wasome kwa bidii.
No comments:
Post a Comment