Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Mwanaidi Ali Khamis akitoa zawadi kwa ajili ya mahabusu ya watoto Mbeya alipofanya ziara ya kukagua uendeshaji wa mahabusu hiyo iliyopo Jijini Mbeya.
Na Mwandishi Wetu, Mbeya
Wananchi
wa Mkoa wa Mbeya na Mikoa jirani wametakiwa kukitumia vizuri chuo cha
Maendeleo ya Jamii Uyole kilichopo Jijini Mbeya ili kuhakikisha
kinawasaidia kufikia malengo na Maendeleo endelevu kwa manufaa yao na
Taifa kwa Ujumla.
Wito
huo umetolewa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto Mhe. Mwanaidi Ali Khamis katika Chuo hicho alipoweka
jiwe la msingi kwenye ujenzi wa madarasa mawili yenye uwezo wa kuchukua
wanafunzi 400.
Mhe.
Mwanaidi amesema Vyuo vya Maendeleo ya Jamii ni msingi wa vijana kuweza
kushirikiana na jamii zao kuibua changamoto na kuzifanyia kazi kutokana
na ujuzi wanaopata.
"Nimejionea
wenyewe wanafunzi wa Chuo hiki vitu wanavyobuni miradi kwa ajili ya
Maendeleo ya Jamii na Taifa katika kutatua changamoto mbalimbali ikiwemo
kujenga vyoo zaidi ya 200 ili kuwaepusha wananchi na magonjwa
mbalimbali ya mlipuko" amesema Mhe. Mwanaidi.
Mhe
. Mwanaidi ameipongeza Idara ya Maendeleo ya Jamii mkoani Mbeya kwa
kushirikiana vyema Chuo hicho na vyuo vingine kwa kuandaa miongozo na
kusisitiza utoaji wa mafunzo unaolenga kuweza kujiajiri na kuajiri
wengine.
"Hili
inadhihirisha kuwa kwa uwepo wa programu za uanagenzi inayofanywa na
wanachuo kujikita katika kuwajengea umahiri katika fani wanazochagua
ambazo zitawasaidia kwenye maisha yao" amesema Mhe. Mwanaidi.
Aidha,
ameutaka uongozi wa Chuo kuhakikisha wanakamilisha ujenzi wa madarasa
hayo yatakayojengwa kwa gharama ya sh. milioni 124 ili kuongeza udahili
wa wanafunzi na kupunguza changamoto ya madarasa chuoni hapo.
Mhe.
Mwanaidi amesema madarasa hayo yatawezesha wanafunzi wengi kujiunga na
Chuo hicho kuwa faida ya maisha yao na Jamii na kwamba Wizara itaendelea
kukiendeleza kwa kutatua changamoto ikiwemo kuongeza mabweni na
kuongeza watumishi kadri fedha itakavyopatikana.
Akizungumza
na watumishi wa Chuo hicho Mhe. Mwanaidi amesema mbali na kuchangia
kuwainua watoto kwa kutoa elimu, Chuo hicho kina umuhimu mkubwa katika
kuchangia Maendeleo ya Mkoa.
Akiwa
chuoni hapo, Mhe. Mwanaidi ametumia fursa hiyo kuwahimiza wananchi
kuendelea kujikinga na UVIKO19 hasa kwa kujitokeza kuchanja ili
kujikinga na madhara ya ugonjwa huo.
Awali,
Mkuu wa Chuo hicho Rajab Sadick akiwasilisha taarifa alisema
wameendelea kupanua wigo Kwa kuongeza udahili wa wanafunzi Kwa asilimia
62.3 tangu mwaka 2018 hadi 2021 ambapo jumla ya wanachuo 1791
wamedahiliwa.
Rajab
ameongeza kuwa, wamedhamiria kutatua matatizo ya vijana kupanga mitaani
kwa kujenga bweni litakalochukua wanafunzi 600 kwa sh. bil 2.8 na
kuiomba Wizara iendelee kusaidia upatikanaji wa fedha.
Kwa
upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mbeya aliyemuwakilisha Mkuu wa Mkoa
katika ziara hiyo, Mhe. Dkt. Rashid Chuachua amemshukuru Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kazi nzuri
anayoifanya katika Mkoa wa Mbeya ambapo wamepiga hatua kubwa ya
Maendeleo katika sekta nyingi.
Akizungumza
Kwa niaba ya wananchi wa kata ya Uyole kilipo Chuo hicho, Diwani wa
kata hiyo Mhe. Daniel Njango amesema Chuo hicho kimeonesha Maendeleo ya
kweli ndani na nje ya Kata ya Uyole ambao watu wa kwanza kunufaika
wamekuwa ni wananchi wa vijiji vya ndani na nje ya kata ya Uyole.
"Chuo
kina ushirikiano mkubwa na Jamii ikiwemo kuwajengea choo bora na ujenzi
wa sekondari, tunahitaji elimu yao kwenye mchango wa Maendeleo ya Jamii
yetu" amesema Diwani hiyo.
Naibu
Waziri Mwanaidi anaendelea na ziara yake Mkoani Mbeya kukagua shughuli
mbalimbali za Maendeleo ya Jamii na kuamsha Ari ya wananchi kujiletea
Maendeleo ambapo katika Jiji la Mbeya ametembelea Mahakama ya watoto na
Mahabusu ya watoto na kuzungumza na watumishi.
No comments:
Post a Comment