HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

October 03, 2021

KUBADILIKA KWA MITAHALA KWA WANAFUNZI KWATAJWA KUWA KIKWAZO CHA UDHOROTESHAJI ELIMU

 


Mgeni rasmi katika mahafali hayo diwani wa kata ya Kyaka ambaye pia ni mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Misenyi Projestus Tegamaisho akitoa  hotuba.

Baadhi ya Wahitimu wa darasa la saba 2021 kutoka Bunazi Green Acres wakisoma risala.
Sehemu ya wazazi walioudhuria mahafali hayo.
 

 

Na Lydia Lugakila,  Misenyi
 

Kauli hiyo imekuja kufuatia risala iliyosomwa na mkuu wa shule ya Bunazi Green Acres iliyopo  wilayani Misenyi Mkoani Kagera Jofrey Moses mbele ya Mgeni rasmi katika mahafali ya 5 ya darasa la saba yaliyofanyika shuleni hapo.

Katika risala hiyo Moses amebainisha kuwa licha ya shule hiyo kujipanga kuboresha taaluma na kuendeleza ufaulu kwa wanafunzi hao bado suala la kubadili mitahala kila mara ni  changamoto  kwani uwachanganya wanafunzi na walimu ambapo baadhi ya mada huonekana kuwa ngumu kwao ikiwemo kutopatikana haraka  kwa vitabu jambo linalosababisha kudhorota kwa huduma ya elimu.

Moses amesema kuwa shule hiyo ina jumla ya wanafunzi 618 ambapo jumla ya wahitimu wa darasa la saba 2021 ni wavulana 35 wasichana 37 ambapo kwa mwaka 2020 shule hiyo ilipata nafasi ya 2 kitaifa huku akiitaja changamoto ya wazazi kutolipa ada kwa wakati kuwa kikwazo pia.

Akijibu risala hiyo Mgeni rasmi katika mahafali hayo diwani wa kata ya Kyaka ambaye pia ni mwenyekiti wa Halmashauri wilaya ya Misenyi Projestus Tegamaisho ameiomba serikali kupunguza kasi ya kubadili mitahala kwani kwa kufanya hivyo hivyo ni kwachanganya wanafunzi na walimu.

"Niiombe serikali itusaidie kupunguza kasi ya kubadili mitahala kila mara hii ni hatari tunao wasomi wengi tunao Maprofesa wakae chini   watafakali na kusikiliza ushauri kwani bado wanazuoni wanalalamikia mitahala ya Sasa"alisema Tegamaisho.

"Kijana anamaliza chuo kikuu anaenda kuendesha pikipiki tunaomba mitahala ijikite wenye ujasiliamali Kama ilivyo kwa wenzetu wa nchi jirani ikiwemo Uganda" alisema mwenyekiti wa Halmashauri hiyo.

Aidha ametumia fursa hiyo kuwa kuwaomba wazazi kujikita katika kufanya kazi ili wapate ada ya kuwalipia watoto wao huku akiwapongeza walimu wa shule hiyo pamoja na waanzilishi kwa namna wanavyopambana hadi kuifanya shule hiyo kunga'ra na kufanikiwa pakubwa.

Hata hivyo kwa upande wake Afisa uhusiano wa shule habari na mawasiliano Respius John amesema ili kuendelea kuboresha taaluma shuleni hapo wamejipanga kuanzisha darasa la Kompyuta ifikapo January  2022, pamoja na kuanzisha maktaba ya kisasa ambayo itawasaidia wanafunzi wa ndani na nje  kupata fursa ya kujisomea vitabu mbali mbali  ili kuwajengea maarifa na ufaulu.

No comments:

Post a Comment

Pages