Mbunge wa Kibaha mjini Silvestry Koka akizungumza na wananchi wa kata ya Mbwawa.
NA VICTOR MASANGU, KIBAHA
Mbunge
wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka ameahidi kuboresha sekta ya
afya kwa wananchi wa kata ya Mbwawa kwa kuweka mipango ya kutenga eneo
maalumu kwa ajili ya ujenzi wa kituo Cha afya.
Koka
ameyasema hayo wakati wa ziara yake ya kikazi katika mkutano wa adhara
kwa wananchi wa kata ya Mbwawa iliyofanyika katika viwanja vya shule ya
msingi Mbwawa na kuhudhuliwa na viongozi mbali mbali wa Chama pamoja na
wakuu wa taasisi mbali mbali.
Katika
mkutano huo Mbunge huyo ambaye pia aliambatana na viongozi wa Chama
alisema kwamba anatambua umuhimu wa afya hivyo atahakikisha
anashirikiana bega kwa bega na Ofisi ya mkurugenzi wa halmashauri ya mji
ili kuanza utekelezaji wa mradi wa kituo Cha afya.
Pia
alisema kuwa anatambua katika kata ya Mbwawa kunahitajika ujenzi wa
kituo Cha afya ili wananchi waondokane kabisa na adha ya kutembea umbari
mrefu kwa ajili ya kufuata huduma maeneo ya mbali.
"Nipo
katika ziara yangu ya kikazi yenye lengo la kusikiliza changamoto mbali
mbali ambazo zinawakabili wananchi ili tuweze kuzifanyia kazi hivyo
nimeanza na wananchi wa kata ya Mbwawa kuwasikiliza,"alisema Koka.
kadhalika
aliongeza kwamba serikali ya awamu ya sita lengo lake kubwa no
kuboresha sekta ya afya kwa wananchi hivyo kwa upande wake atahakikisha
analisimamia kwa nguvu zote ili wananchi wapate huduma ya matibabu bila
usumbufu.
Katika hatua
nyingine aliwahakikishia wananchi wa Mbwawa kuimarisha Hali ya ulinzi na
usalama kwa kuwajengea kituo Cha polisi ili kuondokana kabisa na wimbi
la uharibu.
Pia alisema
ataendelea kuimarisha sekta ya elimu kwa kutenga eneo maalumu kwa ajili
ya ujenzi wa shule ya Sekondari kwa kidato Cha tano na sita.
Akizungumzia
changamoto ya upatikanaji wa maji alisema kwa Sasa bado Kuna mradi
ambao unaendeleaa kutekelezwa lengo ikiwa ni kumtua ndoo ya maji mama
kichwani.
Kwa upande wake
Diwani wa kata ya Mbwawa Judidhi Mloge amemshukuru Mbunge Koka kwa
kutekeleza ilani ya Chama Cha mapinduzi (CCM) kwa vitendo na kumuomba
ujenzi wa kituo Cha afya na ujenzi wa sekondari ya kidato Cha tano na
sita.
No comments:
Post a Comment