Meneja uendeshaji wa miradi kutoka Shirika la Room to Read Tanzania Agripina Kadama akitoa mada wakati wa maadhimisho hayo.
NA VICTOR MASANGU
Wazazi
na walezi wametakiwa kuhakikisha kwamba wanawalinda na kuwatunza watoto
wa kike ikiwemo kuwapatia haki zao zote za msingi pasipo kuwabagua na
kuwapatia stadi za maisha kwa lengo la kuwawezesha kutimiza ndoto zao.
Kauli
hiyo imetolewa na Meneja uendeshaji wa miradi kutoka Shirika la Room To
Read Tanzania Agripina Kadama wakati maadhimisho ya siku ya mtoto wa
kike duniani ambayo yamefanyiika jijini Dar es Salaam kwa kuwashirikisha
wadau mbali mbali.
Alisema
kuwa kwa Sasa watoto wa kike wanatakiwa kuwezeshwa katika Mambo mbali
mbali ikiwemo kupatiwa Hali zake za msingi ikiwa sambamba na kupatiwa
elimu ambayo itawasaidia katika kutimiza malengo yao.
"Tunaadhimisha
siku ya mtoto wa kike duniani lakini kitu kikubwa wazazi na walezi
wanatakiwa kutimiza wajibu wao ipasavyo ikiwemo kuwafuatilia mwenendo
wao pamoja na kuwapa stadi za maisha ili waweze kujitambua"alisema.
Pia
aliongeza kuwa shirika lao kwa Sasa limeweka mifumo mizuri ambayo
itawasaidia kupata elimu hasa kwa wanafunzi wa kuanzia miaka 13 Hadi 17
na kwamba wataendelea kuwasaidia wanafunzi kutoka maeneo mbali mbali.
Kadhalika
alisema kuwa mtoto wa kike anakabiliwa na changamoto mbali mbali
ikiwemo baadhi yao wanajikuta wanakatisha masomo yao kutoka na wazazi au
walezi kuwaozesha wakiwa wadogo.
"Tutaendelea
kushirikiana bega kwa bega na serikali katika kuwasaidia watoto wetu wa
kike kwa kuwapatia maadili mazuri ya kuweza kujitambua zaidi katika
suala zima la kimaisha.
Katika
hatua nyingine alisema kuwa mpaka Sasa mradi huo wameshapita katika
halmashauri mbali mbali hapa nchini na kubainisha kuwa mradi huo
unagusa masuala ya usomaji na maktaba.
Kwa
upande mkuu wa kitengo Cha elimu kutoka Tamisemi Theresia Kuiwite
amesema kwamba serikali itahakikisha kwamba inasimamia Sera zote na
mipango inayuhusiana na elimu.
"Sisi
Kama serikali tutahakikisha kwamba tunaboresha elimu kwa watoto wa kike
pamoja na kutekeleza mipango yote ambayo imewekwa na serikali ikiwemo
suala la kusimamoa Sera ya elimu na stadi za maisha kwa wanafunzi.
Kwa
upande wake mmoja wa wanafunzi kutoka shule ya Sekondari Bundikani Sifa
Mapinduzi amelipongeza shirika la Room to Read Tanzania kwa kumwezesha
kupata mafunzo ya stadi za maisha ambayo yameweza kumsaidia kujitambua
na kukabiliana na changamoto mbali mbali.
Maadhisho
ya siku ya mtoto wa kike duniani kwa mwaka huu kauli mbiu yake inasema
kwamba stadi za maisha ni ufunguo wa ndoto za mtoto wa kike.
No comments:
Post a Comment