HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

October 11, 2021

Tatizo la Afya akili kuongezeka 2030-Waziri wa Afya

 Na Jasmine Shamwepu,Dodoma.


MKURUGENZI Msaidizi Wizara ya Afya anayeshughulikia Magonjwa yasioambukiza Dk.James Kihologwe amesema hadi kufikia mwaka 2030 Tatizo la afya ya akili litaongezeka  na  kufikia asilimia 17 kutoka  asilimia 12 .


Ameyasema hayo jana  jijini Dodoma wakati akimuwakilisha Waziri wa Afya Dk. Dorothy Gwajima kwenye maadhimisho ya siku ya afya ya akili na kupinga matumizi ya pombe kupita kiasi Duniani Octoba 10 ambapo ameeleza afya ya akili ni suala mtambuka katika malezi na makuzi na endapo kila mtu akifanya majukumu yake ipasavyo tatizo hilo litapungua hadi kufikia asilimia 1.


Amesema tatizo la afya ya akili huchangiwa na sababu nyingi ikiwemo na unywaji wa pombe uliopitiliza utumiaji wa madawa ya kulevya ,mawazo Sonona na sababu nyingine nyingi.


"Changamoto  ya pombe na madhara yake ni makubwa ambapo takwimu zinaonyesha tunatatizo kubwa la vifo Milioni 3 vinavyotokana na pombe duniani huku wengine wakiwa na ulemavu wa maisha," Amesema  Dk. Kihologwe. 


Naye Kaimu Mkurugenzi wa Magonjwa yasiokuwa ya kuambukiza kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Njinsia wazee na watoto Dk.Shedrack Makubi amesema Takwimu zinaonyesha Tanzania  kuna wagonjwa wa afya ya akili Milion 7.


"Tunapaswa kuchukua hatua za haraka na kuwekeza zaidi katika Magonjwa ya akili, afya ya akili kwani tatizo hili limeonekana kukua siku hadi siku," amesema Dk. Makubi. 


Kwa upande wake Mbunge wa Shinyanga viti maalumu,Salome Makamba  ameitaka jamii kuamimi kwamba ugonjwa wa akili unatibika na kuacha imani potofu za kuwapeleka wagonjwa kutibiwa kwa waganga wa kienyeji na badala yake wagonjwa wote wenye changamoto  hiyo wapelekwe katika hospitali ya mirembe iliyopo Dodoma. 


"Bado tunachangamoto kubwa katika jamii ni ukweli usiopingika elimu juu ya magonjwa ya afya ya akili ni mdogo na wengi hudhani kwamba ukipata taitizo la akili huwezi kupona jambo ambalo sio la kweli," Amesema  Salome 


"Sasa hivi serikali  ipo kwenye mchakato kupitisha muswada ili iwe sheria ya bima ya afya kwa  kila mtanzania lazima awe na bima ya afya na mimi kama mbunge mwakilishi wa wananchi napendekeza ugonjwa wa akili uingia kwenye matibabu ya bima ya afya,"amesema. 

No comments:

Post a Comment

Pages