HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

October 11, 2021

TUME YA VYUO VIKUU YAONGEZA MUDA WA UDAHILI WA SHAHADA YA KWANZA

 

Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), Prof. Charles Kihampa, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Oktoba 11 wakati akitangaza kuongeza muda wa Udahili wa Shahada ya Kwanza katika Taasisi za Elimu ya Juu nchini kwa Programu ambazo bado zina nafasi kwa mwaka wa masomo 2021/2022.



Dar es Salaam, Tanzania

 

TUME ya vyuo Vikuu Tanzania(TCU), imefungua dirisha la udahili kwa awamu ya nne  kwa mwaka wa masomo 2021/2022 utakaoanza leo Oktoba 11 hadi Oktoba 25 mwaka huu 2021.


Hatua hiyo imekuja baada ya kukamilika kwa udahili wa awamu tatu na kuonekana bado Taasisi za Elimu ya juu nchini kuwa na nafasi katika baadhi ya masomo kwa mwaka huu wa masomo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Oktoba 11,2021  Katibu Mtendaji wa TCU, Profesa Charles Kihampa amesema lengo ni kutoa fursa kwa waombaji ambao hawakuweza kuomba udahili katika awamu tatu zilizopita kutokana na sababu mbali mbali  kupata nafasi hiyo.

" Tume imepokea maombi ya kuongezea muda wa udahili kutoka kwa baadhi ya wa waombaji na Taasisi za Elimu ya Juu nchini ambazo bado zina nafasi katika baadhi ya Programu za masomo kwa mwaka 2021/2022


Aidha Tume imetoa wito kwa Taasisi za Elimu ya Juu nchini zilizoidhinishwa kudahili kwa mwaka huu wa masomo wa 2021/2022 kutangaza programu zile zenye nafasi tu  ili wa waombaji waweze kufanya maamuzi sahihi wakati wakituma maombi na kuepuka usumbufu kwa wao mbaji kuomba programu ambazo hazina nafasi.

“Kama tume pia tunasisitiza vyuo vyote kuzingatia idadi ya wanafunzi iliyoidhinishwa katika programu husika na kwa waombaji wote wanakumbushwa masuala yote yanayohusiana na udahili ama kujithibitisha yawasilishwe moja kwa moja kwenye vyuo na siyo TCU,” amesema Profesa Kihampa

Amewakumbusha waombaji wote kuwa masuala ya yanayohusiana na udahiliama kuthibitisha yawasilishwe moja kwa moja katika vyuo husika na si TCU.

No comments:

Post a Comment

Pages