Waziri wa ujenzi na Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa akingumza Jambo
wakati alipofanya ziara yake ya ya kikazi katika mradi wa ujenzi wa
daraja la mto wami ambapo kwa Sasa umefikia asilimia 61.
Na Victor Masangu, Bagamoyo
WAZIRI
wa Ujenzi na Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa amesema kwamba mradi
mkubwa wa kimkakati wa ujenzi wa daraja kubwa la mto wami unatarajiwa
kukamilika novemba mwaka 2022.
Waziri
huyo pia amemuagiza Mkandarasi anayejenga daraja hilo katika mto Wami
kuhakikisha anaongeza Kasi kwa kuweka mipango ya kufanya kazi masaa 24
ili kukamilisha kazi ya ujenzi huo kwa muda uliopangwa.
Profesa
Mbarawa ametoa agizo hilo wakati alipofanya ziara yake ya kikazi ya
siku moja yenye lengo la kukagua maendeleo ya ujenzi daraja hilo
ambalo kutakuwa ni mkombozi mkubwa kwa wasafiri na wafanyabiashara.
AIdha
aliongea kwamba ujenzi wa daraja hilo ambalo ujenzi wake ulianza Otoba
2018 matatarajio ilikua kukamilika mwezi Septemba 2021 limechelewa
kutokana na changamoto mbalimbali ikiwemo uwepo wa mvua na ugonjwa wa
UVIKO 19
Alimsisitiza
Mkandarasi pia Kujenga daraja hilo kwa ubora unaotakiwa ili lidumu kwa
muda mrefu na kuhakikisha ifikapo Novemba 2022 ujenzi uwe umekamilika.
Waziri
Mbarawa alisema daraja la awali lenye urefu wa mita 88.75 lilijengwa
mwaka 1959 na kwassa lina uwezo mdogo wa kupitisha magari yanayoenda
mikoa ya kaskazini na nchi za jirani kutokana na ongezeko la magari.
Kwa
upande wake Meneja wa Wakala wa barabara Mkoa wa Pwani (TANROADS)
Mhandisi Andrea Kasamwa alisema daraja hilo hadi kukamilika litatumia
kiasi cha Shilingi Bilion .72.
Mhandisi
Kasamwa amesema kuwa daraja hilo jipya litakuwa na urefu wa mita 510 na
upana wa mita 11.85 linajengwa umbali wa mita 670 pembeni ya daraja la
zamani
Aidha alisema tayari Mkandarasi amewasilisha sababu za kimkataba nyongeza ya muda wa Ujenzi kufika mwezi Novemba 2022.
Alisema kazi hiyo ya ujenzi inasimamiwa na makampuni mawili ya Ilshin ya Korea na Advanced Engineering Solution ya Tanzania.
Kasamwa aliongeza kuwa maendeleo ya mradi huo hadi Hadi kufikia Sasa tayari yamekamilika kwa kiasi Cha asilimia 61.4.
No comments:
Post a Comment