HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

October 26, 2021

WILAYA YA MULEBA YAENDELEA KUKABILIANA KUONDOA UVUVI HARAMU

 

Mkuu wa Wilaya ya Muleba, Toba Nguvila.


Kutokana na mwendelezo wa zoezi la kutokomeza uvuvi haramu, kikosi kazi kilichoundwa na Kamati ya Usalama ya Wilaya ya Muleba, Mkoa wa Kagera kimeendelea na doria za mara kwa mara na kufanikiwa kukamata watu wanaojihusisha na uvuvi haramu wakiwa na zana haramu zinazotumika kuvua samaki kiharamu, kokoro na timba zenye thamani ya Tsh. milioni 16 na samaki waliovuliwa kwa kutumia zana haramu hizo tani sita zenye thamani ya shilingi milioni 10.

Akizungumza mara baada ya zana hizo haramu kufikishwa makao makuu ya wilaya, Mkuu wa Wilaya ya Muleba ambae pia ni Mwenyekiti wa kamati ya Usalama ya Wilaya  Toba Nguvila ameendelea kuwasihi wavuvi haramu kuacha mara moja biashara hii kwani itawapelekea kubaya.

"Uvuvi haramu unadhoofisha sana uvuvi endelevu kwenye wilaya ya Muleba na mkoa mzima wa Kagera. Wavuvi hawa mtandao wao ni mkubwa.

Waliokamatwa ni mabingwa wa kuingiza zana haramu kupitia mipaka mbalimbali kutoka nchi za nje ili kuwawezesha wavuvi haramu waliopo ndani ya nchi. Mtandao ni mkubwa sana unahitaji umakini sana kuufutilia, unahitaji nguvu kubwa sana kwaajili ya kuwabaini wote ili kususdi tuweze kukomesha uvuvi haramu ndani ya ziwa Viktoria na ndani ya ziwa Burigi," ameeleza Nguvila.

Aidha, ametoa rai kwa wavuvi wanaojishughulisha na biashara hii haramu kuwa ni vema wakajiunga na uvuvi endelevu, uvuvi wa kihalali kwa kutumia nyavu zilizothibitishwa na Wizara na ambazo hazileti madhara katika mazalia ya samaki. Kwani iko hatari katika uvuvi haramu itakayopelekea kupoteza mazao ya samaki kwenye maziwa, kupoteza ajira kwa waliojiajiri kupitia uvuvi endelevu na kupoteza mapato mengi ambayo Serikali inayapata kupitia Uvuvi endelevu.

Ameendelea kuwaonya wavuvi kuacha kabisa kuvua samaki walio chini ya viwango kwani kikosi kazi kipo kazini na kinaendelea na zoezi la kuwabaini na kuwakamata wote wanaojihusisha na uvuvi haramu.

Hivyo kwa wanaondelea watakamatwa na kufikishwa katika vyombo vya kisheria kwa ajili ya kuchukuliwa hatua kali zinazowastahili ikiwemo kufirisiwa mali zao kwani sheria ya uvuvi ipo wazi.

Ameendelea kueleza kuwa uongozi upo imara na kadri siku zinavyokwenda ndivyo wanavyoongeza nguvu katika kukabiliana na wavuvi haramu kutokana na mtandao wao kuwa mkubwa. Na kuwaomba wananchi kuendelea kutoa taarifa za siri na taarifa wanazotoa zitaendelea kuwa za siri ili kukabiliana kutokomeza uvuvi haramu katika visiwa 39 vilivyopo wilaya ya Muleba ndani ya ziwa Viktoria na ziwa Burigi.

Pia Mhe. Nguvila ameeleza kuwa wapo maafisa uvuvi wanaoshirikiana na wavuvi haramu kuvua samaki kiharamu na kuwasafirisha au kuwauza kiharamu hivyo amewaonya Maafisa Uvuvi hao wasio waadirifu na waaminifu wanaoshirikiana na wavuvi haramu kuendeleza uvuvi huu kuwa watachukuliwa hatua kali za kinidhamu kwani uchunguzi unaendelea.

Mwisho ameomba ushirikiano baina ya wananchi na Serikali ili kutokomeza uvuvi haramu kwa maendeleo na uchumi endelevu wa Taifa letu.

No comments:

Post a Comment

Pages