HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

November 08, 2021

Dkt. Kikwete Mgeni rasmi Usiku wa Tamasha la Vyakale Dhahabu


 
Mkurugenzi wa Kampuni ya Chocolate Princess Mboni Masimba akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es Salaam wakati wa kutangaza rasmi Usiku waTamasha la Vyakale Dhahabu litakalofanyika Disemba 10 mwaka huu.
Mkongwe wa Taarab nchini Afua Suleiman  akitoa pongezi kwa Muandaaji wa Tamasha Hilo Mboni Masimba kwa kuandaa Tamasha Hilo lenye Lengo la kuwapa Burudani wapenzi wa Taarabu.
Malkia wa Taarabu nchini Khadija Kopa akizungumza kuhusu Tamasha la vya Kale dhahabu akiwataka wapenzi wa Muziki wa Taarab kujitokeza kwa wingi huku wakivalia Mavazi ya heshima
 
 
Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam

Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete anatarajiwa kuwa mgeni rasmi wa Usiku wa Tamasha la Vyakale Dhahabu utakaofanyika Disemba 10 mwaka huu katika UKumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Kampuni ya Chocolate Princess ambaye pia ni Muandaji wa tamasha hilo Mboni Masimba amesema usiku huo utafanyika lengo likiwa kusherehekea Miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania.  

" Tamasha hili ni la taarabu asilimia 100  tunakwenda kulitumia kusherehekea miaka ya 60 ya uhuru pia kuwaenzi wakongwe wa muziki wa taarabu hivyo litakaonga nyoyo za wapenzi wa muziki wa mwambao," amesema.

Amebainisha kuwa usiku huo utafanyika kwa ajili ya kuwaenzi wakongwe wa muziki huo akiwemo Issa Matona na Bi Kidude, hivyo Rais wa Awamu ya Nne Dkt. Kikwete atakuwa mgeni rasmi.

Amewataja waimbaji watakaosindikiza usiku huo ni Khadija Kopa, Patricia Hilary, Afua Suleiman, Sabaha Muchacho, Khadija Yusuf, Mzee Yusuf, Abdul Misambano, Ally Star na wengine wengi.

Ameongeza kuwa kiingilio cha tamasha hilo ni Sh elfu 50 ikijumuisha chakula na vinywaji na kwamba wanaume na wanawake wameshauriwa kuvalia mavazi ya Pwani.

Kwa upande wake, Muimbaji Mkongwe wa Taarabu, Khadija Kopa amempongeza Mboni kwa kuandaa tamasha hilo huku akiwasisitiza wapenzi wa muziki huo kujitokeza kwa wingi kupata burudani.

Nae, Mmoja wa Wadhamini wa Usiku huo ambaye pia ni Meneja Masoko wa Kampuni ya K4s Security, Bico Scanda amesema wanayo furaha kuwa sehemu ya tamasha hilo na kuwahakikishia wapenzi wa muziki huo watakuwa  salama na mali zao wakiwa ukumbini humo.

No comments:

Post a Comment

Pages