NA DENIS MLOWE, IRINGA
MGOMBEA
anayepewa nafasi kubwa kuibuka na ubunge jimbo la Iringa Mjini kupitia
Chama cha Mapinduzi, Fadhili Ngajilo amesema atatumia uwingi wa vyuo
vikuu mkoani hapa kuibadilisha Iringa kuchochea maendeleo.
Akizungumza
wakati wa kampeni za jimbo hilo katika kata ya Gangilonga uliofanyika
katika viwanja vya Sabasaba Ngajilo alisema kuwa kupitia vyuo vikuu
tutashirikiana navyo vyema kwani ni chachu ya maendeleo kutokana na
kuzalisha wasomi na wabunifu.
Alisema kuwa
endapo watamchagua kuwa Mbunge atahakikisha anakaa na vyuo mbalimbali
vilivyopo hapa ili kuzungumza namna ya kushiriki katika kuubadilisha
Iringa kwenye sekta mbalimbali kutokana na uwezo katika ubunifu na
kuzalisha wasomi.
Alisema kuwa uwepo wa vyuo
mkoani hapa ni ishara tosha ya mkoa kuwa na rasimali watu ambao
wakitumika vyema katika kubuni mikakati ya maendeleo Iringa itabadilika
kwa haraka.
"Nitahakikisha nashirikiana vyema
na vyuo vikuu kwa kuwa nami nimepita chuo kwa kusoma na kufundisha hivyo
tutakaa nao chini katika kupanga mikakati ambayo itawezesha Iringa kuwa
na maendeleo kwani kule wanazalisha wabunifu ambao wataleta tija katika
maendeleo ya jimbo la Iringa" Alisema
Aidha
Ngajilo aliongeza kuwa kata ya Gangilonga ina uwingi wa benki hivyo
kupitia hilo atahakikisha anatumia vyema uwingi huo kuzungumza na
benki hizo katika mikopo rafiki kwa makundi mbalimbali hasa
wajasiriamali.
Akizungumzia ahadi za mgombea
udiwani wa kata ya Gangilonga Liikotiko Kenyata, Ngajilo alisema kuwa
atahakikisha wanashirikiana kutatua changamoto zote zinazoikabili kata
hiyo.
Kwa upande wake mgombea udiwani wa kata
ya Gangilonga, Likotiko Kenyata alisema kuwa endapo atachaguliwa
atakamilisha miradi ambayo alikwisha ianzisha ikiwemo Milioni 246
kujenga madarasa ya awali manne, jengo la utawala na matundu ya vyoo
katika shule ya Lugalo.
Alisema kuwa atahakikisha anawezesha wananchi kiuchumi , mitaji, na mikopo nafuu na kurasimisha makazi kwenye mtaa wa Lugalo B.







No comments:
Post a Comment