HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

November 11, 2021

UTT AMIS YATOA ELIMU YA FEDHA KWA WANANCHI MAONESHO YA WIKI YA HUDUMA ZA FEDHA DAR


Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Fatma Nyangasa, akisalimiana na Afisa Masoko na Uhusiano wa Kampuni ya Uwekezaji ya UTT AMIS, Waziri Ramadhani, alipotembelea banda la kampuni hiyo wakati wa uzinduzi rasmi wa Wiki ya Maonesho ya Huduma za Fedha katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

 

Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Fatma Nyangasa, akifafanua jambo baada ya kupata maelezo juu ya fursa zinazopatikana katika Kampuni ya Uwekezaji ya UTT AMIS alipotembelea banda la kampuni hiyo wakati wa uzinduzi rasmi wa Wiki ya Maonesho ya Huduma za Fedha katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.


 Afisa Uendeshaji wa UTT AMIS, Chiguru Josiah, akitoa ya elimu ya fedha kwa wananchi waliojitokeza katika maonesho ya Wiki ya Huduma za Fedha iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Afisa Masoko Mwandamizi wa UTT AMIS, Grace Ngailo, akitoa maelezo kuhusu fursa mbalimbali zinazopatikana katika mifuko ya Uwekezaji wa Pamoja.

Afisa Masoko na Uhusiano wa Kampuni ya Uwekezaji ya UTT AMIS, Waziri Ramadhani (wa pili kushoto), akitoa maelezo kwa mmoja wa wananchi waliofika katika uzinduzi rasmi wa Maonesho ya Wiki ya Huduma za Fedha juu ya fursa zinazopatikana katika mifuko ya Uwekezaji wa Pamoja katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Mwananchi akipata maelezo kuhusu mfuko wa Watoto Fund.

No comments:

Post a Comment

Pages