Na Lydia Lugakila , Kyerwa
Wananchi wilayani Kyerwa mkoani Kagera wametakiwa kuimalisha lishe kwa watoto wadogo ili kukuza hali ya ufaulu katika masomo yao.
Wito huo umetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa Rashid Mohammed Mwaimu katika hutoba yake kwenye kikao cha baraza la madiwani lililofanyika wilayani humo.
Mhe. Mwaimu amesema kuwa endapo suala la lishe litazingatiwa katika jamii itasaidia kukuza na kuimalisha afya za watoto kimwili na kiakili na hivyo kufanya watoto kufanya vizuri shuleni kwani lishe mbovu ni moja ya sababu inayosababisha baadhi ya wanafunzi wilayani humo kufanya vibaya katika masomo yao.
‘’Kyerwa tumejipanga kuhakikisha tunadumisha suala la lishe kwa watoto wetu kwani tuna vyakula vingi vya kila aina na vya lishe hivyo ili kuondoa udumavu mtoto na kumfanya afanya vizuri katika masomo yake suala la lishe ni muhimu’’
Mkuu huyo wa wilaya amewahimiza madiwani wa halmashauri hiyo kuwaelimisha wananchi wao juu ya umuhimu wa lishe na kuongeza kuwa mataifa yaliyofanikiwa kiuchumi kwanza yaliwekeza kwenye lishe bora kwa watoto.
Wakati huo huo mkuu wa wilaya hiyo amewataka viongozi wilayani humo kuwahamasisha wananchi kuhakikisha wanashiriki vyema katika zoezi la sensa ya watu na makazi linalotarajia kufanyika mwezi agosti mwaka huu.
‘’Tuhakikishe tunahamashisha ndg zetu bila kuwa na itikadi ili kuhakikisha tunashiriki vizuri katika zeozi la sensa itakapofika viongozi kuanzia kitongoji mpaka ngazi ya juu ili kuruhusu serikali ipange miundombinu ya maendeleo kwa usahihi’’ alisema Mhe. Rashid Mwaimu.
Mhe, Mwaimu amesema kuwa zoezi la sensa lina umuhimu mkubwa kwa nchi kwani unasaidia serikali kujua idadi ya wananchi wake na kupanga kikamilifu miradi ya maendeleo.
No comments:
Post a Comment