Mtumishi wa Mungu Mchungaji Aneth Sebastian akitoa neno katika ibada ya kanisa hilo.
Na Lydia Lugakila, Bukoba
Waumini wametakiwa kuwa na maarifa yaletayo ufunuo ikiwa ni pamoja na kumwamini mwenyezi Mungu.
Kauli hiyo imetolewa na mtumishi wa Mungu Mchungaji Aneth Sebastian wa Kanisa la Makimbilio lililopo Kyabitembe Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera.
Mchungaji Aneth amesema kuwa imani inazaliwa kwa ufunuo hivyo waumini wanatakiwa kuwa na maarifa yenye maoni ikiwemo kuwa na lugha moja.
Mtumishi huyo amesema kuwa maneno ni mengi Ila neno la Mungu linashinda maneno yote na hivyo waumini wanatakiwa kuwa na imani itakayo waletea ushindi katika Bwana.
Hata hivyo ameongeza kuwa ni wakati sasa kwa waumini kujikabidhi mikononi mwa mwenyezi Mungu maisha yao ili kuishi katika ufalme wa Mungu.
No comments:
Post a Comment