Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa mkoani Kagera Rashid Mohamed Mwaimu akizungumza katika Kikao cha Baraza la Madiwani la Halmashauri hiyo.
Na Lydia Lugakila, Kyerwa
Vijana wilayani Kyerwa mkoani Kagera walalamikiwa kushindwa kuzalisha mali kutokana unywaji wa pombe, huku baadhi ya madiwani wa halmashauri hiyo wakipendekeza kutumika kwa viboko.
Kauli hiyo imekuja kufuatia malalamiko yaliyotolewa na diwani wa viti maalum, kutoka kata ya Itera tarafa ya Nkwenda wilayani humo Bi Devotha Biashara katika kikao cha baraza la madiwani kilicholenga kujadili rasmu ya bajeti kwa mwaka wa fedha 2022/2023 kilichofanyika katika ukumbi wa wilaya hiyo.
Katika hoja yake kwa mwenyekiti wa halmashauri hiyo Bi Devotha Biashara amesema kuwa kutokana na wilaya hiyo kujidhatiti katika kilimo cha mazao mbali mbali ikiwemo maharage ndizi na mihogo rika iliyoonekana kufanya kazi ni wazee, huku vijana wakinywa pombe nyakati za asubuhi jambo lilimlazimu kumuomba mkuu wa wilaya hiyo Rashid Mohamed Mwaimu kuelekeza vyombo husika kuhusisha walau adhabu ya viboko kwa vijana watakaobainika katika vilabu vya pombe muda wa kazi.
‘’Mheshiwa mwenyekiti vijana wetu wanashinda kwenye karata hawataki kufanya kazi hata hawataki kujishughulisha na shughuli mbali mbali za uzalishaji mali, niombe mkuu wa wilaya serikali inatenga fedha ili vizazi vijavyo maisha yaweze kuwa mazuri sisi tunazeeka nguvu ya taifa inaisha vijana ndio nguvu zetu, naombeni vyombo husika wakimkuta kijana anakunywa pombe asubuhi kiboko, hana shamba aulizwe kijana una miaka 25 huna shamba huna kazi unazalisha nini ndani ya wilaya yetu hali hii inasikitisha na inatia huruma alisema bi Devotha.
Aidha kwa upande wake mbunge wa jimbo la Kyerwa Innocent Birakwate ameuomba uongozi wa wilaya hiyo kuhimiza vijana kufanya kazi kwani ndio nguvu kazi ya taifa huku akiomba kufuatiliwa kwa vijana hao.
‘’Kwakeli Kyerwa kuna kitu ambacho hakijakaa sawa kwa vijana, vijana tunawapenda lakini kama hatutawahimiza kufanya kazi tunakoelekea ni pabaya sana unakuta saa nne asubuhi kijana yuko baa anakunywa pombe wengine wanacheza bao mimi niombe sana hili jambo lifuatiliwe vijana hao wafanye kazi kwani ndio nguvu kazi ya kesho bila kuwahimiza kufanya kazi mimi naamini hatutaendelea alisema Birakwate mbunge wa jimbo hilo.’’
Hata hivyo akijibu hoja hiyo ya unywaji wa pombe kwa vijana wakati wa kazi, mkuu wa wilaya hiyo Rashid Mohamed Mwaimu amewataka viongozi wilayani humo kushirikiana kutoa taarifa juu ya vijana wote watakaobainika wakinywa pombe wakati wa kazi ili washughulikiwe kwa mujibu wa sheria.
‘’Ukibaini vijana wanacheza pool anakunywa pombe asubuhi toa taarifa mara moja kwenye uongozi ili tumshughulikiemuda huu ni wa kuzalisha mali hatuko tayari kuona mtu akaendelea kulewa kunya pombe hivyo kwa lolote lile juu ya vijana toa taarifa sheria ya vilevi ipo hivyo tushirikiane ili kulinda nguvu kazi yetu’’alisema Mhe Rashid Mwaimu
No comments:
Post a Comment