Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Teddy Njau akizungumza na viongozi wa vitengo wa Shirika la Posta Tanzania wakati akifingua mafunzo ya kuwajengea uwezo wa mfumo wa anauani ya makazi.
Na Asha Mwakyonde, Dodoma
KAIMU Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Teddy Njau amewataka
wananchi,Ofisi pamoja na maeneo yote ya biashara yawe na anuani ya makazi ili kurahisisha zoezi la Sensa ya Watu na Makazi ifikapo mwezi Augosti mwaka huu .
Hayo ameyasema leo jijini Dodoma wakati akifungua mafunzo ya kujengea uelewa viongozi na Watendaji wa Baraza kuu la Shirika la Posta Tanzania amesema utekelezaji wa zoezi anuani ya makazi ni suala la mtambuka.
Amesema utekelezaji wa anauani za unahusisha wadau mbalimbali ikiwemo wizara,Makampuni mashirika Taasisi serikali na zisizo za serikali na wananchi kwa ujumla.
Ameongeza kuwa umeandaliwa mkakati wa utekelezaji unaoainisha majukumu ya kila mdau katika zoezi zima la utekelezaji wa mfumo huo ikiwemo shirika la posta Tanzania.
"Mfumo huo una manufaa mengi na makubwa katika nyakati hizi za ulimwengu wa digitali kurahisisha uapatikanaji,utoaji na ufikishaji wa huduma au bidhaa pale panapo stahiki kuwezesha kufanyika kwa bisahara za kimtandao ikiwa ni pamoja na kuimarisha ulinzi na usalama.
Kaimu huyo ameeleza kuwa mfumo huo wa kidigitali utachangia kutoa fursa kwa vijana kujipatia ajira.
Amesema ni jambo jema kuwajengea uwezo wataalamu kwa lengo la kusimamia uteky wa mfumo huo wa anuani za makazi.
"Tayari wajumbe wa jumuiya za Serikali ya mtaa(ALAT),makatibu Tawala wa mikoa na wakuu wa mikoa wote Tanzania Bara wameshapatiwa mafunzo kama haya kwa lengo la kusimamia utekelezaji wa mfumo huu wa anauani za makazi kwa ufanisi," ameeleza.
Amefafanua kuwa kwa upande wa wataalamu wameweza kuwapa mafunzo wataalamu wa tehama na maafisa mipango miji ramani kutoka Halmashauri zote nchini Tanzania Bara na Zanzibar ambapo walianzimia mpango kazi wa utekelezaji wa mfumo huo katika maeneo yao.
Kaimu posta Masta mkuu Macrice Daniel ameeleza kuwa wameona ni kuwakutanisha viongozi wakuu waposta katika mafunzo ya mfumo wa anuani ya makazi kwa kuwa Ni mustakabali wa taifa.
No comments:
Post a Comment