HABARI MSETO (HEADER)


January 31, 2022

UWEKEZAJI WA HALAIKI UNAVYOINUA KIPATO CHA WATANZANIA


Kuna namna nyingi za uwekezaji, kilimo na misitu, madini, uvuvi, masoko ya fedha na mitaji hii ni mifano michache tu.  Kupitia halaiki wawekezaji na makampuni  wanaweza waka changisha pesa kutoka watakao jitokeza kutoka kwenye jamii kwa ajili kufanya biashara, au kampeni dhidi ya jambo fulani, au mradi fulani. Cha muhimu hapa ni kwamba mtaji utatoka kutoka kwenye jamii na huu mtaji unakuwa kwa ajili ya lengo fulani. 

 

Si jambo la ajabu siku hizi, tunasikia kibubu, au pengine jumuia Fulani ya uwekezaji, vikundi mbali mbali vyote vikiwa na nia moja kuweka na kuwekeza fedha kwa ajili ya kuboresha Maisha. Pesa ndiyo kila kitu, wengi tunase,a hivyo. Wapo wanao sema – pesa sabuni ya roho. Wakati mwingine pia jamii hukusanya pesa zisaidie mambo ya kheri au hata majanga. Cha muhimu hap ani nguvu ya Umoja.

Kwa hivyo basi, kwa dhana hii wote mbali mbali, makampuni, taasisi mbali mbali zinakusanya fedha pamoja  kwa lengo Fulani. Wakusanyaji wanakuwa ni watu tofauti tofauti wenye elimu na uzoefu mbali mbali jambo ambalo ni muhimu kwenye kutimiza lengo la kukusanya pesa hizo, iwe msaada kwa wengine, uwekezaji, au ujenzi katika jamii.

 

Katika hali ya kawaida, inaonekana kama jambo jamii, lakini kumbuka katika wanadamu kila mtuna tabia yake, hakuna binadamu wanaofanana tabia na kila kitu,  hivyo kuna changamoto ya kukusanya vichwa vingi na kuvifanya viwe na mtizamo mmoja.

 

Ili watu wawekeze Pamoja, au wachangie kwenye kapu moja ni lazima kuwa na lengo ambalo ni bayana, wazi kwa kila mtu na lengo hilo liwe na faida au matarajio mazuri kwa jamii. Mfano uwekezaji wa Pamoja kupitia mifuko ya UTT AMIS. Lengo lake ni kukusanya fedha na kuziwekeza ili kuwapa wawekezaji wa fedha hizo faida shindani. Hivyo hapa lengo laweza kuwa faida ambayo mwekezaji anaipata kama gawio au kama faida kwenye biashara ingine ile.

Faida za jamii kuungana na kufanya uwekezaji kwa ajaili ya lengo Fulani ni nyingi ikiwemo kupunguza gahara za uwekezaji. Kwa mfano ili kuabiashara ya mtaji wa milioni 10, mkiwa wawili kila mtu atotao shilingib milioni 5, mkiwa wan ne kila mtu atato shilingi milioni 2.5. Kwa mifuko ya UTT AMIS hakuna gharama. Unajaza fomu unapata akaunti ya mfuko husika unaanza kuwekeza.

Nguvu ya mtaji. Kwa mradi unao hitaji pesa nyingi, ni vigumu kwa mtu wa kawaida kumudu gharama zake.  Kwa mfano ili kununua hati fungani mwekezaji anapaswa kuwa na walau shilingi milioni 1, pia akaunti za muda maalumu ni kuanzia shilingi mia tano, shilingi miliono moja, laki tanu kama mtaji ni hela ndogo lakini bado ni hela nyingi kwa mwananchi wa kipato cha chini; kwenye uwekezaji wa Pamoja mtaji ni kuanzia shilingi elfu 10, na watu wakichanga Pamoja pesa zinakuwa nyingi, pesa zikiwa nyingi kwa Pamoja wanaweza wekeza mabilioni iwe kwenye akaunti za muda maalumu, au hata kwenye hati fungani, na pengine kwenye majengo, vyombo vya usafiri na sehemu nyingine nyingi.   

Ubalozi, mkiwa wengi kwenye uwekezaji kila mtu anakuwa balozi wa huo uwekezaji, kampuni kubwa zenye wawekezaji wengi, zinajikuta wawekezaji wenyewe wakivutia wawekezaji wengine kwa njia ya mazungumzo tu kupitia madaraja mbali mbali. Hii inapunguza gharama za kutafuta masoko, wawekezaji Pamoja hutumia njia mbali mbali licha ya mzangumzo ya uso kwa uso, njia hizo ni kama vile simu, tovuti, mitandao kama Facebook, Instagram, twitter nakadhalika.

 

Wachangiaji wa mtaji, watapata riba, au watakuwa wamiliki wa mradi, au watakuwa sehemu ya mradi. Au hawatapata chochote zaidi ya kutambulika na heshima kutoka kwa jamii ambayo michango yao imetumikia.

katika hili la mwisho ina maana mchangiaji alitoa kama msaada. Kwa hiyo uchangiaji unaweza ukawa kwa sababu ya faida za kiuchumi au misaada ya bure kwa ajili ya maendeleo.

Kuna mambo makubwa matatu; wachangiaji ni wengi, ni lazima kuwe na daraja litakalo kutanisha wenye kutoa na wenye kupokea pesa, na ni lazima kuwe na tamko lililo wazi la kutaka watu washiriki kwenye uwekezaji wa namna hii.

Mwisho wa siku ni kuwa huu ni mfumo ambao waliokusanya  pesa kwa  wanakutanishwa kupitia kwa msimamizi na  wanao hitaji hizo pesa kwa makubaliano maalumu  ili kupata manufaa fulanina zaidi ikiwa faida.

Uwekezaji wa pamoja kwenye mifuko ya uwekezaji huwa na tabia kama hii lakini hapa watu wanaweka kwa masharti husika na kwa madhumuni ya kupata faidi.

Kwenye uwekezaji wa pamoja  wenye pesa watatoa watampa meneja  awekeze kweny sehemu walizo kubaliana aidha kwenye baadhi ya  kampuni zilizo orodheshwa kwenye Soko La Hisa la Dar es salaam,  au kampuni binafsi yenye uhitaji , pia kukopesha benki kupitia akaunti za muda maalumu na   kukopesha serakali kupitia hati fungani za muda mfupi au  za muda mrefu.

 

Mifuko ya uwekezaji wa pamoja kwa ajili ya uwekezaji wa kukopesha  hapa fedha zinakusanywa kwa madhumuni ya uwekezaji kwenye kukopesha tu, kabla ya kukopesha mambo mengi yatafanyiwa tathmini ikiwemo uwezo wa mkopaji kulipa, uaminifu wa mkopaji, historia ya mkopaji, muda wa mkopo, riba, na kama kuna mashaka yoyete kwa mkopaji na mwenendo wa uchumi wa wakati wa kukopesha na matarajio ya baadae. Hili ni jambo ambalo linafanyika ki utaalamu huku tahadhari za hali ya juu zikichukuluwi kuhakikisha kuwa hatari zote za uwekezaji wa namna hii umezingatiwa. Mifuko ya uwekezaji wa pamoja kama  mfuko wa wa Ukwasi na ule wa Hati Fungani yote inayo simamiwa na UTT AMIS ni mfuko ambayo imekuwa ikitoa  faida nzuri kwa wawekezaji na pia ni mifano mizuri kama chombo cha serekali ambacho kupitia uwekezaji wa pamoja  hukusanya pesa kutoka kwa jumuia kwa madhumuni ya kuzikopesha kwenye sehemu tathiminiwa kwa uhakika wa kiasi kikubwa kuwa faida itapatikana.

 

Pia kuna mifuko ya uwekezaji wa pamoja kwa ajili ya kuwekeza kwenye soko la hisa kwa hapa kwetu kampuni zilizo orodheswa kwenye soko la hisa la Dar es salaam.  Mifuko inayowekeza kwenye hisa ni mifuko ambayo inaweza lipa san kama meneja anaye simamia uwekezaji atakuwa amewekeza kwenye kampuni ambazo zina ufanisi wa hali ya juu unaopelekea kampuni hizo kupata faida nzuri. Hisa zinalipa sana haswa pale mwekezaji anapokuwa hana haraka ili kuzipa nafasi ya kukabiliana na change moto za kupanda na kushuka aidha kwa kampuni fulani au kwa soko lote la hisa. Kimsingi uwekezaji kwenye hisa kama uwekezaji kwenye sehemu nyingine unahitaji utaalamu na wakati mwingine uvumilivu ni muhimu sana. Hisa zinam panda na kushuka au tunasema mwendo wake unategemea pamoja na mambo mengine mwendo wa soko.

Ili kupata faida ya soko la hisa na mitaji basi mwekezaji anaweza chagua mfuko wenye mchanganyiko. Yani kwa aslimia fulani unawekeza kwenye hisa, na asilimia nyingine kwenye mabenki na kwenye hati fungani. Kwa kufanya hivi tunasema mwekezaji ametawanya athari za uwekezaji, kwa kupitia uwekezaji anuai yaani hajaweka mayayi yote kwenye kapu moja.

 

No comments:

Post a Comment

Pages