HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 02, 2022

Rais Samai: watendaji wa Mahakama tendeni haki


 

Na Asha Mwakyonde, Dodoma

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan amewataka Watendaji wa Mahakama Nchini kuendelea kutenda haki kwani bado kuna malalamiko kwa baadhi ya wananchi kucheweleshewa haki na wakati mwingine kunyimwa kabisa haki hasa kwa wanawake wajane kuhusu masuala ya mirathi.


Rais Samia ametoa wito huo leo Jijini Dodoma wakati akifunga kilele cha maadhimisho ya siku ya sheria nchini kuashiria kuanza kwa Kalenda ya mahakama kwa Mwaka huu iliyohudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Serikali,Viongozi wa Dini pamoja na Wananchi yanayoenda Sambamba na kaulimbiu isemayozama za mapinduzi ya nne ya viwanda safari ya maboresho kuelekea Mahakama mtandao.

"Kwa bahati mbaya Sana serikali haina Mamlaka yakutoa haki bila kutegemea Mahakama itoe haki na hapa nisisitize nyie mnaofanya kazi  ya mahakama ambao mnatakiwa kutoa haki lazima mtende haki,"

Aidha amesema Serikali Itawaunga Mkono Kikamilifu Mahakama katika matumizi ya Teknolojia za Kisasa za TEHAMA ili Kukabiliana na Uchumi wa Kisasa katika Kufanikisha Lengo hilo  ambapo ni Lazima Kuboresha Sheria kwani Mapinduzi ya Viwanda yamesababisha mabadiliko ikiwemo Mfumo Wa Elimu Za Vyuo Vikuu Wanafundishwa Kukabiliana na Mapinduzi hayo kupitia mifumo hiyo.


Hata hivyo amesema wataliangalia suala la upungufu la uhaba wa watumishi wa mahakama ikiwemo usafiri pamoja na vitendea kazi ili kuiwezesha Mahkama katika utendaji kazi wake na kufanya suala la  uwekezaji katika Mahakama mtandao .

Kwa upande wake Spika wa Bunge Tulia Ackson amemshukuru Rais  kwa kumuamini kwa nafasi hiyo yakuwa Spika wa Bunge huku akitoa  wito kwa wananchi kushiriki kutoa maoni yao katika utungwaji wa Sheria hasa pale wanapotoa matangazo kuhusu kuwepo kwa Muswada mpya.

Awali Jaji Mkuu wa Tanzania,Profesa Ibrahim Juma akaeleza changamoto mbalimbali ikiwemo  matumizi madogo ya uwekezaji katika muhimili wa mahakama hasa katika suala laTEHAMA,upungufu wa watumishi pamoja na suala la akili bandia katika mahakama.


Kwa upande wake Mwanasheria Mkuu wa Serikali,Jaji  Dk.Elieza Feleshi akaeleza shughuli za Mahakama ikiwemo kuunguliwa kwa Mashauri ya kimahakama  kwanjia ya mtandao na kuomba kuongezewa bajeti kwa mwaka huu wa fedha.


Naye Rais wa Chama cha wanansheria cha Tanganyika (TLS),DK.Edward Hosea sekta ya sheria ijizatiti kufanya maboresho ya utoaji haki hasa katika suala la utoaji taarifa sahihi kwakutumia huduma mtandao pamoana utoaji wa elimu kwa wananchi  juu ya ubongo bandia katika utoaji haki .

No comments:

Post a Comment

Pages