HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 21, 2022

SIKU YA AFYA YA BENKI YA CRDB YAPONGEZWA

Naibu waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi ,Ajira na Vijana, Patrobasi Katambi (mbele kushoto) akichuana kwenye mchezo wa riadha na Meneja wa CRDB Tawi la UDOM, Machaku Geni walipofungua bonanza la michezo kwa wafanyakazi wa wafanayakazi benki hiyo Kanda ya Kati yenye Mikoa ya Morogoro,Iringa,Dodoma na Singida ,michezo hiyo ilifanyika mwisho wa wiki Jijini Dodoma.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Ajira, Vijana, Kazi na Wenye Ulemavu, Patrobas Katambi a
lisema hakuna shughuli yayote ya kiuchumi ambayo inaweza kufanyika kwa ufanisi kama mtu hana afya njema na kusisitiza haja ya kushiriki mazoezi na kubadilisha mienendo ya maisha
Baadhi ya wafanayakazi wa matawi ya benki hiyo Kanda ya Kati yenye Mikoa ya Morogoro,Iringa,Dodoma na Singida ,michezo hiyo ilifanyika mwisho wa wiki Jijini Dodoma wakimsikiliza geni rasmi Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Ajira  na Vijana, Patrobasi Katambi.
Meneja Kanda ya Kati, Chabu Mishwaro alisema wanatumia fursa hiyo kiwakutanisha wafanyakazi kutoka mikoa minne ya Kanda ya Kati ambao pamoja na kuangalia afya zao wanakutana kubadilisha mawazo.
Meneja Kanda ya Kati, Chabu Mishwaro akipimwa afya na Muuuguzi wa Hospital ya Rufaa ya Dodoma ,Sceva Madeha (kulia) akimpima presha.
Muuuguzi wa hospital ya Rufaa ya Dodoma ,Sceva Madeha (kulia) akimpima presha Naibu waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi ,Ajira na Vijana ,Patrobasi Katambi alipofika kufungua bonanza la wafanyazi wa Benki ya CRDB lililoshirikisha wafanayakazi wa matawi ya benki hiyo Kanda ya Kati yenye Mikoa ya Morogoro,Iringa,Dodoma na Singida ,michezo hiyo ilifanyika mwisho wa wiki Jijini Dodoma ,nyuma Lake ni Meneja wa CRDB Kanda ya Kati Chabu Miswaro.
Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya CRDB Kanda ya Kati wakishiriki michezo kwenye bonanza lililowashirikisha wafanyakazi hao kutoa Mikoa ya Singida,Morogoro ,Iringa na Dodoma na bonanza hilo lilifanyika uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma mwisho wa wiki 
Meneja Ustawi wa Afya ya Mfanyakazi, Ujumuishaji na Uwezeshaji kutoka Makao Makuu ya Benki ya CRDB, Crescensia Kajiru akizungumza na kusema Siku ya Afya ya CRDB imelenga kuboresha afya ya wafanyakazi na kusisitiza kuwa kipaumbele cha benki ni afya.
***********
WANANCHI wametakiwa kushiriki katika michezo mbalimbali ambayo itawajenga kiafya na kua na ari nzuri ya kufanya kazi na shughuli za uzalishaji mali.

Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Ajira, Vijana, Kazi na Wenye Ulemavu, Patrobas Katambi ameyasema hayo na kuongeza kua afya njema ndio mtaji wa kwanza mtu binafsi na taifa.

Katambi ameyasema hayo wakati wa kuongoza mazoezi ya wafanyakazi wa Benki ya CRDB  Kanda ya Kati ikiwa ni kuadhimisha Siku ya Afya ya CRDB iliyofanyika katika Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.

Alisema hakuna shughuli yayote ya kiuchumi ambayo inaweza kufanyika kwa ufanisi kama mtu hana afya njema na kusisitiza haja ya kushiriki mazoezi na kubadilisha mienendo ya maisha.

"Dunia ya leo kila siku watu wanapisha kutafuta fedha, lakini ninyi mmeamua kutumia Siku hii Kwa ajili ya masuala ya afya ina maana CRDB mnaelewa masuala ya fedha kwasababu mtaji wa kwanza kwa uchumi wa mtu binafsi au Taifa ni afya njema."

Pia amehimiza wafanyakazi na jamii kuendelea kupima afya kila wakati ikiwa ni pamoja na magonjwa yasiyoabukiza na yale ya kuambukizwa kama Ukwimu na kutunza afya kwa kufanya mazoezi na kubadilisha mtindo wa maisha.

Meneja Ustawi wa Afya ya Mfanyakazi, Ujumuishaji na Uwezeshaji kutoka Makao Makuu ya Benki ya CRDB, Crescensia Kajiru alisema Siku ya Afya ya CRDB imelenga kuboresha afya ya wafanyakazi na kusisitiza kuwa kipaumbele cha benki ni afya.

" Tunajua majukumu yetu muda mwingi tunautumia kwa kukaa na huwezi kupata muda wa mazoezi ndio maana tuko hapa kukumbushana kuwa mazoezi ni muhimu.

" Hivyo katika matawi yetu kuna haja ya kutenga muda wa mazoezi na kukumbushana namna ya kula chakula na kuondokana na mtindo wa maisha unaoleta magonjwa yasiyoya ya kuambukiza ambayo uwezo wa kuyakabiri uko mikononi mwetu."

Kajiru alisema utaratibu wa kupima afya na kufanya mazoezi uemkuwa ukifanyika kwenye Kanda sita ikiwemo Ofisi ya Burundi na kuwa mpaka mwisho wa mwezi Machi mwaka huu utaratibu huo utakamilika.

Kwa upande wake Meneja Kanda ya Kati, Chabu Mishwaro alisema wanatumia fursa hiyo kiwakutanisha wafanyakazi kutoka mikoa minne ya Kanda ya Kati ambao pamoja na kuangalia afya zao wanakutana kubadilisha mawazo.

No comments:

Post a Comment

Pages