HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 21, 2022

PSC simamieni maadili ya kazi- Katambi

 Na Mwandishi wetu

 

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira,Vijana na Wenye Ulemavu)  Mhe.Patrobas Katambi ameitaka Tume ya Utumishi wa Umma (PSC) kusimamia taratibu na maadili ya kazi ili kuepusha ajali na watu kupata ulemavu katika maeneo yao ya kazi.

 

Mhe. Katambi ameyasema hayo leo wakati akishuhudia makabidhiano ya kompyuta za mezani zilizotolewa na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) kwa Tume ya Utumishi wa Umma Nchini (PSC) ili kutatua changamoto za kiutendaji na kuongeza ufanisi ili kuleta maendeleo nchini.

 

“Tume ya Utumishi wa Umma ofisi yenu ni muhimu sana kwa maendeleo ya nchi, salama yetu yote iko kwenu,kuanzia watu kutekeleza wajibu uliokusudiwa ule wa viapo au usiwe wa viapo na uwe wa mikataba au usiwe wa mikataba katika kuutumikia umma wa watanzania, msimamie mikataba kwani watu wakiwajibika tutapunguza madhara mengi zaidi, amesema Katambi.

 

Aidha amesema kuwa kuwezeshwa kwa Tume iyo  na WCF kutaiwezesha Tume hiyo kufanya kazi kwa kutumia mifumo ya kisasa ya TEHAMA na kutaboresha  utendaji kwani kwa kutumia mifumo ya TEHAMA kutapunguza urasimu, kutaleta uwazi, kutapunguza upendeleo na kuongeza uwajibikaji.

 

Aidha ameipongeza WCF kwa ushirikiano wake na Tume ya Utumishi wa Umma kwa kuonyesha mfano bora wa kuisaidia vitendea kazi tume iyo na kuwasisitiza kuendelea kushirikiana katika kutoa huduma bora kwa watanzania na kulinda haki za wafanyakzi na stahiki zao.

 

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) Dkt. John Mduma amesema katika kutekeleza majukumu yao mfuko huo umeendelea kushirikiana na Taasisi mbalimbali zikiwemo Sekta ya umma na Binafsi ili kutatua changamoto za kiutendaji kwa lengo la kuongeza tija na maendeleo nchini.

 

“WCF inatambua umuhimu wa Tume hii katika kusimamia uwajibikaji nchini hususan watumishi wa umma na usimamizi wao madhubuti utachangiwa sio tu na uweledi wa wafanyakazi wa Tume katika utekelezaji wa majukumu yao bali pia uwepo wa vifaa vitakavyorahisisha utekelezaji wa majukumu yao” ameongea Mduma

 

Naye Katibu wa Tume hiyo Bw.Mathew Kirama ameishukuru WCF kwa kuiunga mkono Tume katika katika kuongeza ufanisi wa majukumu yake.

“Kitendo hiki ni cha upendo na mshikamano na hatutawaangusha na tutaona namna bora ya kuhudumia mfuko huu na taasisi zote za umma kwa ujumla, asante sana kwa kutushika mkono katika eneo hili la kuimarisha mifumo ya TEHAMA”amesema Kirama.

 

No comments:

Post a Comment

Pages