HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 09, 2022

TIMU ZA NEC NA TRA ZATOANA JASHO JIJINI DODOMA

 

NEC FC wakishangilia moja ya mabao waliyofunga dhidi ya TRA FC
Wachezaji wa pande zote mbili wakichuana. 
Familia ya NEC QUEENS ikiwa katika picha baada ya mchezo.
Mchezo ukiendelea 
Mchezo wa mpira wa Pete baina ya NEC QUEENS (jezi nyeupe) dhidi ya TRA QUEENS ukiendelea.
***********
Na Mwandishi wetu
TIMU za NEC Spots Club ile ya mpira wa Miguu ya NEC FC na Mpira wa Pete NEC Queens leo zimeshuka katika dimba la Sekondari ya John Melin iliyopo Miyuji jijini Dodoma kucheza michezo ya kirafiki na timu za TRA FC na TRA Queens.

Michezo hiyo yua kirafiki ya kujiandaa na michuano ya Mei Mosi inayotaraji kuanza mwezi huu jijini Dodoma iliziwezesha timu hizo mbili kutambua mapungufu na ubora wa vikosi vyao.

Kwa upande wa mchezo wa Mpira wa Pete Timu ya NEC Queens ilicharaza bila huruma watoza ushuru wa TRA Queens kwa pete 18-14. Mabao ya NEC Queens yalipachikwa na Sophia Mpema na Tully Kihaka wakati yale ya TRA yakifungwa na Subira Kasutu na Magreth John. 

Soka upepo haukua mzuri kwa NEC FC ambapo walikubali kichapo cha mabao 6-3 kutoka kwa mabingwa mara mbili mfululizo wa michuano ya Mei Mosi watoza kodi wa TRA FC. Bao zote tatu za NEC FC zilipachikwa kiamini kwa ufundi mkubwa na Nahodha wa timu hiyo, Omar Mgunda na kuibuka nyota wa mchezo. 

Mabao ya wapinzani wao TRA FC yalipachikwa wavuni na Hiram Ntabudyo aliyefunga bao mbili, huku bao moja kila mmoja yakifungwa na Koshuma Mohamed, Ezra Mbise, Mayele Gasaya na Nehemia Mkane. 

Timu za NEC Sports Club zinataraji kushuka dimbani tena mwishoni mwa wiki kumenyana na timu ambazo zitatajwa hapo baadae.

No comments:

Post a Comment

Pages