BENKI
ya NBC imezindua Kampeni ya ‘Jaza Kibubu Tusepe’ itakayojikita kwenye
utoaji wa elimu kwenye masuala ya kifedha itakayoambatana na zawadi
chungumzima kwa wateja wake.
Akizungumzia
wakati wa uzinduzi wa Kampeni hiyo jijini Dar es Salaam leo Aprili 6
2022, Abel Kaseko, Mkuu Bidhaa na Mauzo kwa Wateja Binafsi, amesema
kuwa kampeni hiyo itakuwa ya miezi sita na kwamba wateja wa NBC
watanufaika za kampeni hiyo.
Kaseko amesema kuwa kampeni hiyo itadumu kwa muda wa miezi sita na kwamba elimu itatolewa sambamba za zawadi .
Amesema
kuwa wateja 80 wa benki hiyo watashinda tiketi za kushuhudia mchezo wa
watani wa Jadi Simba na Yanga utakaochezwa kwenye kiwanja cha Mkapa
jijini Dar es Salaam.
Akifafanua
juu ya kushikiri kwenye kampeni hiyo Dorothea Mabonye Meneja wa Bidhaa
kwa wateja Binafsi amesema kuwa mteja wa Benki hiyo atakayeweka kiasi
cha laki tatu kwa kudunduliza kuanzia leo tarehe 6 mpaka tarehe 24
Aprili 2022 atapata nafasi ya kushinda tiketi ya kushuhudi mchezo wa
huo wa watani wajadi.
Amesema
kuwa wateja 50 kutoka kutoka mikoa mbalimbali nchini watazawadiwa
tiketi ya kuhudhuria kwenye mtanange huo utakachezwa tarehe 30 Aprili na
kwamba washindi hao watagharamiwa Chakula na malazi wakiwa jijini.
Mabonye amesema kuwa wateja 30 kutoka jijini Dar es Salaam watazawadiwa tiketi ya VIP kwenye mchezo huo.
Mbali
na zawadi hiyo Mabonye ameeleza kuwa kutakuwa na tiketi za washindi
watano wa safari ya kushuhudia fainali za kombe la dunia nchini Qatari
Desemba mwaka .
Mabonye
amesema kuwa kutakuwa na kundi la mwanzo la washindi wa safari hiyo
ambao watadunduliza kwenye akaunti zao za NBC kiasi cha Shilingi Milioni
1 kuanzia leo tarehe 6 mpaka Mwezi Septamba.
“Kundi
la pili litawahusu wateja wetu watakaoweka kwa kudunduliza kiasi cha
shilingi milioni saba kwenye akaunti zao kuanzi leo tarehe 6 Aprili
mpaka mwezi Septemba , kundi hili litakuwa linawashindi wawili
watakaozawadiwa tiketi za safari ya Qatari, malazi, vyakula na vinywaji
na kushuhudia mechi kwenye fainali za kombe la dunia . Hawa watapata
tiketi za mzunguko”,amesema Mabonye.
Mabonye ametoa wito kwa watanzania kufungua akaunti kwenye benki hiyo ili kunufaika na kampeni hiyo.
No comments:
Post a Comment