Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Dkt. John Jingu akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kikao cha Baraza la Wafanyakazi la Wafanyakazi la Tume ya Taifa ya Uchaguzi leo 31 Machi, 2022 jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Dkt. Wilson Mahera Charles akipongezana na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Dkt. John Jingu baada ya kufungua kikao cha baraza la Wafanyakazi la Tume ya Taifa ya Uchaguzi leo 31 Machi, 2022.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi., Dkt. Wilson Mahera Charles akifafanua jambo wakati wa kikao hicho cha Baraza kilichokutana leo tarehe 31 Machi, 2022 jijini Dodoma. Katikati ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Dkt. John Jingu na kulia ni Katibu wa Baraza la Wafanyakazi la Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Livini Morrice.
Sehemu ya wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Tume ya Taifa ya Uchaguzi wakiwa katika kikao cha baraza kicho kutana leo tarehe 31 Machi, 2022 jijini Dodoma.
Sehemu ya wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Tume ya Taifa ya Uchaguzi wakiwa katika kikao cha baraza kicho kutana leo tarehe 31 Machi, 2022 jijini Dodoma.
Sehemu ya wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Tume ya Taifa ya Uchaguzi wakiwa katika kikao cha baraza kicho kutana leo tarehe 31 Machi, 2022 jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi., Dkt. Wilson Mahera Charles akifafanua jambo wakati wa kikao hicho cha Baraza kilichokutana leo tarehe 31 Machi, 2022 jijini Dodoma.
Mgeni Rasmi Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. John Jingu akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Baraza la wafanyakazi la Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
Na Mwandishi Wetu
“Watendaji mkiamua kutekeleza majukumu yenu
vizuri, kwa kuzingatia tija, na uwajibikaji ni dhahiri tija itaonekana kazini
na mtaweza kuwarahisishia viongozi wenu kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi
mkubwa,” amesema Dkt Jingu.
Akizungumzia umuhimu wa kikao hicho, Dkt
Jingu aliwataka wajumbe wa baraza la wafanyakazi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi kutambua
kuwa baraza hilo ni kiungo muhimu katika kukuza ustawi na maendeleo ya Tume,
hivyo wahakikishe kuwa wanawawakilisha wenzao ambao hawapo kwenye kikao hicho
kwani wana mategemeo makubwa kutoka kwao.
Aidha Katibu Mkuu amewapongeza viongozi na
watumishi wote wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa kuchapa kazi kwa ufanisi
mkubwa, na pia amewapongeza aliyekuwa Mwenyekiti Mstaafu wa Tume ya Taifa ya
Uchaguzi Mhe Jaji Semistocles Kaijage ambaye muda wake wa kuwa mwenyekiti wa
Tume umemalizika na Mhe Jaji wa Mahakama ya Rufani Jacobs Mwambegele kwa
kuteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
Naye Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi wa
Tume ya Taifa ya Uchaguzi ambaye pia ni Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume, Dkt
Wilson Mahera Charles aliwataka wajumbe
wa baraza hilo kutambua dhamana waliyopewa ya kuwa kiungo kati ya uongozi na
watumishi wa Tume.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge
na Uratibu) Dkt John Jingu amewataka watumishi wa umma nchini kuongeza ufanisi
na uwajibikaji katika sehemu zao za kazi ili tija iweze kuonekana katika
utekelezaji wa shughuli zao.
Akifungua kikao cha baraza la wafanyakazi wa
Tume ya Taifa ya Uchaguzi kilichofanyika leo jijini Dodoma, Katibu Mkuu
amewakumbusha watumishi wa umma agizo alilolitoa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan jana wakati akipokea ripoti ya TAKUKURU na ile
ya Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali ya kuzingatia weledi,
uwajibikaji na tija katika sehemu zao za kazi.
Dkt Jingu amesema kila mtumishi wa umma
amepewa nafasi ya kutekeleza majukumu yake kulingana na vipaji na sifa za
weledi wake katika kazi hivyo amewataka watumishi hao kwenda kutimiza majukumu
yao kama inavyotarajiwa.
No comments:
Post a Comment