Na Jasmine Shamwepu, Dodoma
BARAZA
la Mawaziri wa Nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki
zinatarajia kukutana kabla ya mwisho wa mwaka huu kutangaza kuongezeka
kwa muda wa kuanza kutumika sarafu moja kwa nchi zote za Jumuiya.
Nchi
zinazounda Jumuiya wanachama ni pamoja na Tanzania, Kenya, Uganda,
Rwanda, Burudi, Sudani kusini na Kongo ambayo imemaliza mchakato wa
kujiunga hivi karibuni
Akizungumza
na wandishi wa habari jana jijini hapa Mwenyekiti wa Wabunge wa Bunge
la Afrika Mashariki Adam Kimbisa alisema hatua ya kutumia sarafu moja ni
muhimu katika kurahisisha biashara kwani itasaidia kuondokana na
utaratibu wa kubadili fedha Kila unapovuka mpaka kwenda nchi nyingine.
"Majadiliano
ya itifaki ya umoja wa fedha yalikamilika mwaka 2013 ambapo nchi
wanachama zilikubaliana kuwa na kipindi Cha maandalizi Cha miaka 10
kuanzai mwaka 2014 na inatarajia kukamilika ifikapo 2024 na BARAZA la
Mawaziri litakuta hivi karibuni kwà ajili ya kuongeza muda kwasababu bado
mchakato haujafika kwenye hatua ambayo kufikia mwaka kesho kutwa
itakuwa imekamilika,"alisema
Kimbisa
alisema bunge la Afrika Mashariki limetunga sheria mbili za kuanzisha
taasisi za Jumuiya zitakazosimamia mchakato wa umoja wa fedha na pia
inaendelea na miswada mingine inayolenga kuanzisha taasisi
zitakazosimamia utekelezaji wa umoja wa fedha.
Katika
hatua nyingine Kimbisa alisema mtangamano wa afrika Mashariki ni katika
shirikisho la kisasa ambapo hatua hiyo inalenga kuona Jumuiya ikiwa
nchi moja yenye mfumo wa shirikisho ambao utasaidia kuongeza nguvu
katika nyanja zote za kufanya kuwa wamoja zaidi.
Alisema
katika kufikia hatua hiyo zipojuhudi zili"zofanywa ikiwemo kuanzisha
vyombo kama bunge la Afrika Mashariki, mahakama ya afrika Mashariki,
mashirikiano katika masuala ya ulinzi na usalama na katika sera ya mambo
nje.
UMOJA WA FORODHA
Kwa
mujibu wa Kimbisa alisema hatua ya umoja wa forodha ilianza rasmi mwaka
2005 baada ya nchi wanachama kuridhia itifaki ya umoja wa forodha na
bunge la Afrika Mashariki ikatuka sheria ya kusimamia ambapo imesaidia
kufungua milango ya biashara Kwa kuondoa ushuru wa forodha Kwa bidhaa
zonazozalishwa ndani ya Jumuiya.
Alisema
wananchi wanakuwa na uhuru wa kupeleka bidhaa zao katika nchi yoyote
ambaye ni mwanachama bila vizuizi imesaidia kuongeza ukubwa wa Soko na
ubora wa bidhaa kutokana na ushindani.
SOKO LA PAMOJA.
Kuhusu
utekelezaji wa Soko la pamoja Kimbisa alisema mambo mbalimbali
yamefanyika ambayo yameleta matokeo makubwa ya maendeleo ya Jumuiya
ikiwemo uanzishwaji wa vituo 15 vya huduma za pamoja mipakani.
Alitaja
juhudi nyingine kuwa ni utekelezaji wa himaya moja ya forodha,
kuongezeka Kwa biashara ya ndani ya Jumuiya kutoka dola bilioni 1.6 Kwa
mwaka 2005 hadi dola bilioni 3.2 mwaka 2020 na kuongezeka Kwa mitaji na
Uwekezaji katika Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Kimbisa
alisema mafanikio yaliyopatikana kutokana na soko la pamoja ni kutolewa
Kwa vitambulisho Kwa raia wa nchi wanachama, fursa za masomo ,
kufunguliwa Kwa fursa za ajira,baadhi ya nchi zimeondoa ada ya vibali
vya kazi, kutolewa Kwa pasi moja ya kusafiria , kuondolewa Kwa vikwazo
visivyo vya kiforodha, na kuanzishwa Kwa mamlaka ya ushindani Kwa nchi
za Afrika Masharik.
"Fursa
zinahitaji watu wazichangamkie ili ziweze kuwaletea matunda watanzania
tunapaswa kuzichangamkia fursa hizo Kwa kushindana na raia wa nchi
nyingine wanachama ili tuweze kunufaika na mtangamano wetu na tafiti
zinaonyesha kuwa moja ya vikwazo vinavyosababisha wanachama wengi
washindwe kuzichangamkia fursa ni kutokuwa na uelewa wa
kutosha,"alisema.
Kwa
upande wake Mbunge Tanzania katika bunge la Afrika Mashariki kutoka
Zanzibar Maryam Ussy Yahya alisema katika Jumuiya hiyo wamependekeza
jina la sarafu hiyo itakayotumika na nchi za umoja wa nchi za Afrika
msahariki iitwe shilingi ya Afrika Mashariki.
Aidha
aliwataka watanzania kuendelea kuchangamkia fursa ya Soko la Afrika
Mashariki ambapo hadi Sasa idadi imefikia watu milioni 270 hivyo ni
uthibitisho tosha kuwa Kuna fursa za kutosha.
Tanzania
inawakilishwa na Wabunge tisa katika bunge la Afrika Mashariki ambao ni
Adam Kimbisa, Dk.Ngwaru Maghembe, Maryam Ussi Yahya, Dk. Abdullah
Hasnuu, Josephine Sebastian Lemoyan na Fancy Nkuhi.
No comments:
Post a Comment