HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 07, 2022

Rais Samia ashiriki Maadhimisho Siku ya Karume Day Kisiwandui Zanzibar

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, akiwa katika Dua ya pamoja na Mama Mariam Mwinyi, Mama Mbonimpaye Mpango na aliyekuwa Mke wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar Mama Fatma Karume katika Kumbukizi ya miaka 50 ya aliyekuwa Rais wa kwanza wa Zanzibar Hayati Sheikh Abeid Amani Karume leo tarehe 07 Aprili 2022 Afisi Kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM Kisiwandui Zanzibar.

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiwa na Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Ali Mwinyi wakielekea katika Kaburi la aliyekuwa Rais wa Kwanza wa Zanzibar Hayati Sheikh Abeid Amani Karume leo tarehe 07 Aprili 2022 Afisi Kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM Kisiwandui Zanzibar ikiwa ni kumbukizi ya Miaka 50 tangu kifo chake.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiweka Shada la Maua katika Kaburi la aliyekuwa Rais wa Kwanza wa Zanzibar Hayati Sheikh Abeid Amani Karume leo tarehe 07 Aprili 2022 Afisi Kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM Kisiwandui Zanzibar ikiwa ni kumbukizi ya Miaka 50.  

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiwa na Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango, Rais Mstaafu wa Zanzibar Mhe. Amani Abeid Karume, Mkuu wa Majeshi  Jenerali Venance Mabeyo, wakiomba Dua mbele ya Kaburi la Rais wa kwanza wa Zanzibar Hayati Abeid Amani Karume leo tarehe 07 Aprili 2022 Afisi Kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM Kisiwandui Zanzibar ikiwa ni kumbukizi ya Miaka 50 tangu kifo chake. 

 


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akizungumza  na  Rais Mstaafu wa Zanzibar Amani Abeid Karume, na Makamu wa Rais Dkt. Philip Isdor Mpango baada ya kukamilika kwa Dua ya kumbukizi ya kutimia miaka 50 tangu kifo cha Rais wa kwanza wa Zanzibar Hayati Abeid Amani Karume iliyofanyika leo tarehe 07 Aprili 2022 Afisi Kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM Kisiwandui Zanzibar. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiagana na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa baada ya kukamilika kwa Dua ya kumbukizi ya kutimia miaka 50 ya kifo cha Rais wa kwanza wa Zanzibar Hayati Abeid Amani Karume iliyofanyika leo tarehe 07 Aprili 2022 Afisi Kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM Kisiwandui Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

Pages