Balozi wa zaidi ya miaka 25 katika tarafa ya Korogwe Mjini Mika Mwirongo akifurahi kumuona Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Abdulrahman Kinana kwenye mkutano uliyofanyika katika ukumbi wa Lembeni
mjini Korogwe.
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi
(CCM) Tanzania Bara, Abdulrahman Kinana amewataka madiwani na wabunge
kukataa kupitisha miswada ya Sheria yenye kukandamiza haki na kuminya
fursa ya wananchi wanyonge kujiendeleza kiuchumi.
Pia,
amesema Sasa ni wakati muafaka kulitazama vyema kundi la
wajasiriamali wadogo wakiwemo mamalishe na bodaboda ili wawekewe
mazingira mazuri ya kunufaika na juhudi zao.
Kinana
ameyasema hayo leo mjini Korogwe, wakati akizungumza na wana CCM katika
ukumbi wa Lembeni, akiwa katika ziara ya kukagua uhai wa Chama na
kujitambulisha kwa wanachama.
"Madiwani
nyinyi ndio mnaosimamia sheria za Halmashauri, mkiona sheria hazina
uhusiano na wananchi kataeni. Mkiletewa sheria pelekeni kwa wananchi
waulizeni, rahisisheni maisha ya watu muwasidie wakue.
"Wabunge
wa Bungee la Jamhuri ya Muungano...sheria ikija bungeni waambieni
(serikali) kwa sasa hatuipitishi mpaka tukashauriane na wananchi,"
alisema.
No comments:
Post a Comment