HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 26, 2022

Mvua kubwa Kesho

Na Irene Mark

WAKAZI wa mikoa ya Dar es Salaam, Tanga, Pwani vikiwemo visiwa vya Mafia, Unguja na Pemba wametakiwa kuchukua tahadhari ya mvua kubwa itakayonyeesha kesho Aprili 26.2022.

Mvua hiyo inayotarajiwa kunyesha kwenye maeneo mengi ya mikoa tajwa ikiwa ni muendelezo wa mvua za masika zilizotabiriwa kwenye marejeo ya utabiri kutokana na mabadiliko ya tabia nchi.

Taarifa ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), iliyotolewa leo Aprili 25.2022 imetahadharisha kuwepo kwa mvua kubwa hivyo kuzitaka mamlaka husika na wananchi kuchukua tahadhari na kusafisha maeneo yao kuzuia kutuwama kwa maji.

Pamoja na tahadhari hiyo, TMA imetoa angalizo la mvua kubwa kwa baadhi ya maeneo ya Mkoa wa Lindi kesho Aprili 26.2022.

TMA pia imetoa angalizo la mvua kwa mikoa ya Tanga, Dar es Salaam, Pwani vikiwemo visiwa vya Mafia, Pemba na Unguja kwa siku mbili kuanzia Aprili 27 hadi 28.2022.

Kwa mujibu wa tahadhari hiyo wakazi wa maeneo husika wametakiwa kuzingatia taarifa za hali ya hewa na kuchukua hatua ili kuepusha athari zinazoweza kutokea.

No comments:

Post a Comment

Pages