HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 26, 2022

Mavunde afungua studio, wasanii kurekodi bure


Na Mwandishi Wetu, Dodoma


NAIBU Waziri wa Kilimo na Mbunge wa Dodoma Mjini, Anthony Mavunde amefungua studio ambapo wasanii mbalimbali jimboni humo watarekodi bure.


Mavunde amesema hayo jana katika Tamasha la Furaha Moyoni, kililopambwa na Kwaya ya El Shaddai ya jijini humo na kuongeza kuwa lengo la kuanzisha studio hiyo ni kuwasaidia wasaniii wa Dodoma Mjini.

Amesema hiyo ni fursa ya kipekee kwa kwaya zote zilizopo Jimbo la Dodoma Mjini kwenda kurekodi katika studio hiyo bila malipo.


"Hiyo ni huduma yangu kwenu na ni bure kabisa kwa sababu hiyo studio nimeianzisha kwa ajili yenu. Ningependa pia tuwe na matamasha makubwa ya kumsifu Mungu kupitia Kwaya mbalimbali kama ambavyo imekuwa leo na nipo tayari kusaidiana nanyi kuandaa haya matamasha makubwa na kuwatafutia wadhamini," amesema Mavunde.

No comments:

Post a Comment

Pages