Mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Pwani Hawa Mchafu Akizungumza Jambo wakati wa mafunzo hayo yaliyoandaliwa kwa ajili ya madiwani wanawake wa Mkoa wa Pwani.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge akifunga mafunzo hayo ya siku mbili kwa madiwani wanawake wa Mkoa wa Pwani.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wakiwa katika wameketi kwa ajili ya kusikiliza mafunzo hayo.Ofisa jinsia wanawake na watoto wenye ulemavu kutoka kituo cha
sheria na haki za binadamu Gutruda Dyabene akifafanua Jambo katika
magunzo hayo.
Na Victor Masangu, Kibaha
Mbungu
wa viti maalumu Mkoa wa Pwani Hawa Mchafu kwa kushirikiana na kituo cha
Sheria za haki za binadamu wameandaa mafunzo ya siku mbili kwa
madiwani wa Mkoa wa Pwani lengo ikiwa ni kuwajengea uwezo katika
utekelezaji wa majukumu yao na kukabiliana na changamoto zinazoikabili
jamii.
Mafunzo
hayo ambayo yamefungwa Leo na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge
ambaye alikuwa mgeni rasmi katika ufungaji wa mafunzo hayo ambayo
yamehudhuliwa na madiwani wapatao 54 kutoka halmashauri mbali mbali.
Katika
hotuba yake Kunenge aliwata madiwani hao kuhakikisha kwamba
wanatekeleza majukumu yao ipasavyo ikiwemo kuwatumikia wananchi kwani
wao ndio wamesabisha kuwa viongozi hivyo wanapaswa kuwatumikia.
"Madiwani mnatakiwa kuhakikisha mnajituma ili mlete matokeo chanya katika kutatua kero na changamoto
mbali mbali za wananchi na kuweza kusimamia ipasavyo miradi mbali
mbali ya maendeleo iliyopo katika maeneo yenu,,"alisema Kunenge
Aidha
Kunenge aliwasisitiza madiwani hao kuweka mipango ya kupigania haki za
watoto ,kukemea mimba za utotoni na Mila na desturi ambazo Ni kandamizi
ili kupunguza matukio ya aina hiyo ndani ya jamii.
Kwa
upande wake mbunge wa viti maalum Mkoa wa Pwani, Hawa Mchafu alisema
kutokana na matukio ya Mila na desturi zisizo rafiki kwa watoto wa
kike,utoro mashuleni na mimba na ndoa za utotoni katika mkoa huo ndicho
kilichomsukuma kutafuta ufadhili ili madiwani wapate mafunzo hayo.
Alisema ,amealika madiwani wote 56 wanawake kwa mkoa huo ambao wamejitokeza Ni 54 ambapo Ni sawa na asilimia 96.4.
”
Nampongeza Kunenge ,nampongeza na kumshukuru Rais Samia kwa Kuwa
wanamaendeleo wa kwanza Mkoani Pwani, Namshukuru Rais kwa kuhakikisha
Tisa za bweni zinazotakiwa kujengwa nchini mojawapo itajengwa Mkoani
hapa “
”
Ujenzi wa shule hizi utakwenda kupunguza mimba za utotoni ,watoto
wanapaswa wasome katika Mazingira bora na ya kuwalinda ili kuhakikisha
wanasonga kupata taaluma Yao “alisema Mchafu.
Mchafu ,aliwashauri madiwani wanawake kujifunza kuwekeza kabla ya kukoma nafasi zao za Uongozi ilihali wawe na pa kuanzia.
Nae
ofisa wa Jinsia (wanawake, watoto na wenye ulemavu kutoka kituo cha
haki za binadamu ,Gutruda Dyabene alieleza wametoa mafunzo ya siku mbili
ili kujadili changamoto za Uongozi wanazopata madiwani wanawake pamoja
na nanma gani wanaweza kuthubutu kugombea nafasi mbalimbali kama ilivyo
kwa wanaume.
Alisema
baada ya mafunzo,wataandaa mipango kazi katika Halmashauri zao kufanyia
kazi eneo la wanawake, mimba za utotoni,na utoro.
Diwani viti maalum Mjini Kibaha ,Selina Wilson alisema mafunzo hayo yatakwenda kuwasaidia katika majukumu yao .
Aliomba
mkuu wa mkoa wa Pwani , kuzungumza na vyombo vya ulinzi na Usalama
maana baadhi ya wananchi wanakwama maeneo hayo Mara wanapotaka Sheria
itende haki katika kesi za mimba za utotoni na unyanyasaji wa kijinsia.
No comments:
Post a Comment