Na Lydia Lugakila, Karagwe
Wananchi katika kata ya Kihanga wilayani Karagwe Mkoani Kagera wamediliki kutumia vyakula ikiwemo unga ili kujihami na tembo ambao wameendelea kuvamia kata hiyo kwa kuharibu mazao ya wananchi pamoja na athari nyinginezo.
Akizungumza na Habari Mseto Blog, kwa niaba ya wananchi hao, diwani wa kata ya Kihanga, Rwamuhangi Stivin amesema kuwa mnamo April 3 hadi 4 tembo hao kwa makundi wameendelea kuvamia mashamba ya wananchi akiwemo Raulent Bwangamu, Samson Samweli na Christopher na kisha kuharibu mazao yakiwemo maharage, mahindi,karanga miwa huku wakijihami kwa kurusha unga na chumvi ili kuepuka tembo hao kutopitisha mkonga ndani ya nyumba na kuleta madhara kwani tembo hupenda vyakula hivyo .
Hadi Sasa tembo hao wanasadikika kuweka makazi yao katika kijiji cha mramba karibu na kambi ya wachina ambapo diwani huyo ameeleza kusikitishwa na msaada toka mamlaka husika kuchelewa huku wananchi wakiendelea kupata shida.
Aidha amesema kuwa TANAPA wameisha ahidi kufika maeneo hayo kusaidiana na wananchi kuwathibiti wanyama hao ambapo pia ameiomba serikali kuona namna ya haraka ya kuwasaidia kujenga kituo ili askari wa wanyama pori awe karibu kwa msaada zaidi.
Hata hivyo mwaka 2020 tembo walivamia kata hiyo na kuua Baba,mama na mtoto huku mama wa familia huyo naye kufariki dunia kutokana na mshtuko.
No comments:
Post a Comment