HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 02, 2022

SERIKALI MKOANI KAGERA YAAHIDI MAKUBWA KWA WAWEKEZAJI BINAFSI SEKTA YA ELIMU

Na Lydia Lugakila, Bukoba

Serikali mkoani Kagera imeahidi kuendelea kutoa ushirikiano kwa wawekezaji binafsi wanao wekeza katika sekta mbalimbali za maendeleo  kwa ajili ya manufaa ya watanzania.

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Wilaya ya Bukoba mkoani wa Wilaya ya Kagera, Moses Machali (pichani) alipokuwa mgeni rasmi katika sherehe za kuwaaga wahitimu wa kidato cha sita wakati wa  mahafali ya tano Shule ya Sekondari Kemebos na mahafari ya sita Shule ya Sekondari Kaizirege yaliyofanyika katika viwanja vya shule hizo ambapo mkuu huyo wa wilaya amesema wanakagera wanapaswa kuacha majungu na kupeana  ushirikiano katika shughuli mbalimbali za kuwaletea kipato.

 Hata hivyo mhe, Machali amewasihi wazazi mkoani kagera kuwalea watoto kwa maadili na nidhamu  na kuwekeza vyema katika elimu ili kuwatengenezea misingi imara katika maisha yao huku akiwataka kutowalea watoto kizembe

Akisoma risala ya wahitimu wa shule za Kaizirege na Kemebos Elina Emanuel amesema kuwa wameeandaliwa vyema kuelekea mitihani yao ya kuhitimu inayotarajiwa kufanyika kuanzia mei 9 mwaka huu na shule zao zinatarajia kushika nafasi za juu kitaifa kama ulivyo utaratibu wa shule hizo tangu zianzishwe.

Kwa upande wake meneja wa shule hizo, Eulogius Katiti amesema kuwa mkurugenzi wa  taasisi hizo yupo   kwenye mpango wa kuanzisha chuo kitakacho hudumia  sehemu kubwa ya vijana katika mkoa wa kagera na Tanzania kwa ujumla.

No comments:

Post a Comment

Pages