HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 02, 2022

JESHI LA POLISI KANDA MAALUM YA DAR ES SALAAM LIMEWAKAMATA WATUHUMIWA 20 KWA TUHUMA MBALI MBALI ZA KIJINAI


Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam linaendelea na jitihada za kuzuia vitendo vya kihalifu kwa kufanya Oparesheni maalum kali zinazoongozwa na taarifa fiche dhidi ya Uhalifu na Wahalifu.

 

Polisi imemkamata Mohamed Omary, Miaka 27, Nyamwezi, mkazi wa Chamazi kwa tuhuma za kushiriki katika matukio ya unyang’anyi wa Pikipiki kwa waendesha Bodaboda kwa kushirikiana na wenzake, Athuman Abdallah, miaka 29, Mzaramo mkazi wa Yombo na Hassan Twaha @Dangote,miaka 21, Msambaa Mkulima wa Mtongani Temeke

Mbinu ambayo wahalifu hao wamekuwa wakiitumia katika unyang’anyi wa Pikipiki hizo ni kumtumia mwanamke mmoja ambaye hujifanya mjamzito aliyefahamika kwa jina la Aziza Hamza miaka 21 Mndengereko, Mkazi wa Yombo ambaye hukodi bodaboda mpaka walipo wenzake kwa ajili ya kupora pikipiki. Tukio la uporaji likikamilika wahalifu hao huzipeleka pikipiki hizo kwa Omary Salum@ Miaka 30, Ndengereko, mkazi wa Tandika, Kilimahewa ambaye kazi yake ni kutoa GPRS/ ving’amuzi kwa pikipiki zenye ving’amuzi.   Athuman Mohammed Bakari @ BOKO, miaka 42, mkazi wa Kilwa Kivinje yeye hujihusisha na  kuzitafutia kadi na kuziuza katika  mikoa ya Mtwara na Lindi.

 

Jeshi la Polisi limefanikiwa kumkamata Sophia Musa, miaka 28, mkazi wa Toangoma ambaye ndiye mpokea maombi ya kutengeneza kadi toka kwa *boko* na baadae kumpelekea Ibrahimu Ally miaka 31, Mrangi mkazi wa Buguruni ambaye hufanya kazi ya kudurufu kadi hizo za Pikipiki.

 

Katika katika upekuzi watuhumiwa hao wamekutwa na Pikipiki tatu (3) za wizi,

1.  MC 292 DCE

2.  MC 733CEG na

3.  MC 250 DBF

Kadi za pikipiki (9) Kadi za Gari (11), vyeti vya kuzaliwa, vyeti vya kumaliza elimu ya sekondari, stika za mamlaka ya mapato (TRA) na stika za Baraza la Mitihani vyote vinachunguzwa.

 

 

Katika tukio lingine, Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es alaam linamshikilia Ally Mussa (36) Mluguru mfanyabiashara kwa tuhuma za kutoa taarifa za uongo kwamba alinyang’anywa pesa Kiasi cha Tsh 8,000,000 maeneo ya Temeke Mwembe Yanga wakati  akizipeleka Bank ya CRDB Temeke Sterio,ambako alidai  ghafla alivamiwa na watu sita wakiwa kwenye pikipiki tatu na mmoja akiwa na silaha ndogo walimshambulia na kumpora pesa hizo zilizokuwa ndani ya begi.

 

Jeshi la Polisi lilifanya uchunguzi wa kina wa tukio hilo na ilibainika  kuwa hakukuwa na unyang’anyi wa kutumia silaha bali ilikuwa ni tukio la kutengenezwa na mtoa taarifa, ilibainika pesa zile alipewa na tajiri wake kuzipeleka bank  na njiani aliingiwa na tamaa akatapeliwa  baada ya  kutaka kupata  pesa  US Dollar kwa kubadilishana na pesa alizokuwa nazo. Mtuhumiwa huyo atafikishwa mahakamani kwa kutoa taarifa za uongo kwa afisa wa Serikali.

 

Pia Jeshi la Polisi Kanda Maaluma Dar es salaam linashirikiana na Mamlaka ya Mapato (TRA) ili kubaini wamiliki wa Pikipiki nane (08) zilizokuwa zinatumiwa na watu wanaotuhumiwa kuwa waporaji wa mikoba katika maeneo mbalimbali ya jiji maarufu kama vishandu ambao walikimbia na kuzitelekeza Pikipiki hizo wakati wanafuatiliwa.

Pikipiki hizo zina  namba za usajili

1.     MC.928 CWC, BOXER,

2.     MC. 685 CRR BOXER,

3.     MC. 304 DCR BOXER,

4.     MC78 …AP FEKON( *Plate namba imekatwa )

Pamoja na Pikipiki nyingine nne ambazo hazina usajili zina chasisi namba tu ambazo

5.     MD2B15BY3LWK85620* BOXER,

6.     MD2A21BY4KWA96154* BOXER, 

7.     MD2A21BY5JWH87188* BOXER na

8.     Pikipiki ya nane(08) Chasis zake zimefutwa.

 

Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es salam limewakatamata watu 8 kwa tuhuma za uvunjaji  na wizi katika maeneo ya Kimara, Mabwepande, Mbweni na Kinondoni, vitu walivyokutwanavyo  ni ,  Tv mbili aina ya lg inch 43 na inch 32, TV aina ya aboder inch 21, home theater aina ya samsung yenye spika mbili, deki ya sumsung, laptop aina ya hp,  Tv  aina ya samsung inchi 62, tv (02) zenye ukubwa wa inchi 42 aina ya samsung na na tv aina ya  tlc (02) zenye ukubwa wa inchi 32, TV ya Star Times na mobisol (1) na Computer mpakato (01) aina ya Dell tv 0,TV aina ya lg inchi 32.

 

Taratibu za kisheria zinakamilishwa ili watuhumiwa hao wafikishwe Mahakamani

 

Katika hatua nyingine  Jeshi limekamata  wezi wawili wa magari  wakiwa na Gari ya wizi aina ya Suzuki Cary yenye Chasis namba DA52T128686 .  Gari hilo liliibwa tarehe 27/03/2022  Upelelezi ulifanyika na tarehe 29/03/2022 watuhumiwa hao walikamatwa pamoja  na gari hilo.

 

Kuhusu madawa ya kulevya , Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es salam limemkamta Kasimu  Ally, Myao, 22yrs, islam, biashara na mkazi wa Kimara Suka, akiwa na Magunia manne (4) ya bangi  kwenye nyumba anayoishi mtuhumiwa huyo. Mtuhumiwa atafikishwa mahakamani baada ya taratibu za kisheria kukamilika.

 

HALI YA USALAMA KUELEKEA MECHI YA KLABU YA SIMBA VS USGN JUMAPILI

 

Jumapili ya tarehe 3 Aprili kwenye uwanja wa Benjemin Mkapa kutakuwa namchezo wa soka wa  kimataifa Kombe la Shirikisho la Afrika baina ya klabu ya Simba na USGN ya Nigeria utakaochezwa saa 04 :00 usiku. Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam yayari limejipanga kuhakikisha usalama unaimarishwa kwa kiwango cha juu.kwa  mashabiki na wachezaji, Ulinzi ndani na nje ya uwanja utakuwa katika kiwango cha juu .

Jeshi la Polisi Kanda maalum ya Dar es salaam linatoa tahadhari  kuwa mtu yeyote atakayebainika kujihusisha na vitendo vilivyo kinyume na sheria au taratibu  ndani au  nje ya uwanja atashughulikiwa  kwa mujibu wa sheria

Jeshi linawashukuru wananchi wanaoendelea kutoa taarifa mbalimbali za wahalifu na uhalifu, Tunaahidi kuzitunza  siri hizo  kwa lengo la  kuzuia vitendo vya uhalifu.

No comments:

Post a Comment

Pages