Meneja wa Tanzania Commercial Bank (TCB), Tawi la Mbagala Edward Mwoleka (katikakati), akifanyiwa kipimo cha moyo na Mtaalam kutoka Alliance insurance Group Ravi Kumar, wakati Tanzania Commercial Bank waliposhirikiana na Alliance insurance kutoa vipimo vya magonjwa mbalimbali kwa wakazi wa mbagala na viunga vyake bure anaeshuhudia ni Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Alliance Insurance Group, KVA Krishnan. Hafla hiyo imefanyika leo katika ofisi za Tanzania Commercial Bank Tawi la Mbagala jijini Dar es Salaam.
Meneja wa Benki ya Tanzania Commercial Bank Edward Mwoleka (wapilikushoto), pamoja na Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Alliance Insurance Group, KVA Krishnan (kulia), wakiangalia mmoja ya wakazi wa Dar es Salaam, Joeseph John, akipatiwa huduma ya kipimo cha moyo na Mtaalam kutoka Alliance Insurance Group Ravi Kumar, wakati Tanzania Commercial Bank waliposhirikiana na Alliance insurance kutoa vipimo vya magonjwa mbalimbali kwa wakazi wa mbagala na viunga vyake bure bila malipo
Baadhi ya wananchi waliojitokeza ili kupata vipimo hivyo. Meneja wa Tanzania Commercial Bank Tawi la Mbagala Edward Mwoleka(Kulia), akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Alliance Insurance Group, KVA Krishnan na wakati wa hafla maalum ya utoaji vipimo bure uliyodhaminiwa na Tanzania Commecial Bank kwa kushirikiana ikishirikiana na Shirika la Bima Alliance Insurance incorporation kwa wakazi wa Dar es salam. Mkazi wa Mbagala akifanyiwa kipimo cha shinikizo la damu na Mtaalamu kutoka Shirika la Bima Alliance Insurance incorporation Group Ravi Kumar,kwakushirikiana na Tanzania Commercial Bank walipokuwa wakitoa huduma ya vipimo vya magonjwa mbalimbali kwa wakazi wa Mbagala na vitongoji vyake bila malipo. Meneja wa Tanzania Commercial Bank (TCB), Tawi la Mbagala Edward Mwoleka akishuhudia mmoja wa wakazi wa jiji la Dar es Salaam akipata kipimo cha sukari kutoka kwa Mtaalamu wa Maabara Husna Hassan wakati Benki ya Tanzania Commercial Bank ilipoungana na kampuni ya bima ya Alliance kutoa vipimo vya uchunguzi kwa wakazi wa Mbagala na vitongoji vyake bila malipo.
Dar es Salaam, Tanzania
Mamia ya wananchi leo
wamejitokeza kupima afya zao bure Tanzania Commercial Bank tawi la
Mbagala iliyopo Halmashauri ya Manispaa ya Temeke ikiwa ni sehemu ya Tanzania
Commercial Bank pamoja na shirika la bima la Alliance Insurance Corporation
kujali wateja wao na wananchi kwa ujumla.
Akizungumza katika
hafla hiyo Meneja wa Benki ya Tanzania Commercial Bank Tawi la Mbagala Edward
Mwoleka “Amesema kuwa kila mtanzania angependa kujua afya yake hivyo
Tanzania Commercial Bank imeamua kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya
sita chini ya Rais Mama Samia Suluhu Hassan hasa katika sekta ya afya kwa kutoa
huduma ya vipimo bure bila malipo yoyote kwa wananchi wa mbagala.na viunga
vyake”.
“Benki ya Biashara ya
Tanzania tuna kila sababu ya kuwajali watanzania na kuwapa wanachotamani ndio
maana leo tumeungana na wenzetu wa Alliance Insurance Corporation kwa kutoa
huduma ya kufanya vipimo vya magonjwa mbalimbali bure”.
Mwoleka
amewataka watanzania na wakazi wa Mbagala kujiunga na Benki ya TCB kwani
imekuwa ikitoa huduma bora na rafiki kwa kila mtanzania pamoja na kujali jamii
ya wananchi.
“Tuna mikopo ya
kuanzia Mfanya Biashara mdogo, wa kati na hadi mkubwa hivyo niwasihi wateja
wetu wajitokeze kuja kupata huduma katika benki yetu pendwa”.
“Pia tuna mikopo ya
wastaafu hivyo amewasihi wastaafu kujitokeza na kujiunga kwenye fursa hizi. Pia
Benki inatoa mikopo mingi mbalimbali yenye masharti nafuu na rafiki”.
Kwa upande wake
Msemaji wa Alliance Insurance Justin Erick ameishukuru Tanzania Commercial Bank
kwa kuwaamini na kufanya kazi pamoja ili kuhakikisha wanatoa huduma bora kwa
wananchi.
Ameongeza kuwa kwa
huduma zote za bima zinapatikana katika matawi yote ya Tanzania Commercial Bank
hivyo amewasihi wananchi wa Mbagala wajivunie uwepo wa Alliance Insurance kwani
ni kampuni ya kwanza na ubora Tanzania katika utoaji wa huduma.
No comments:
Post a Comment