HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 05, 2022

UVIWADA yahimizwa kusajili wanachama zaidi

Na Mwandishi Wetu

 

SERIKALI imewataka wamiliki wa vituo vya watoto wadogo na shule za awali kujisali ili kupewa miongozo ya kuendesha vituo hivyo na mitaala kwa ajili ya walimu wa shule za awali.

Akizungumza wakati wa sherehe za uzinduzi wa Umoja wa Vituo vya Kulelea watoto mchana na shule za awali (UVIWADA), Kamishna Msaidizi wa Ustawi wa Jamii kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Baraka Makona alisema vituo vingi vinatumia mtaala wa awali na wengine wanatumia wa nje ya nchi hivyo inawafanya watoto hao kutokuwa na mwendelezo mzuri.

“Nilikuwa Moshi, Kilimanjaro nikakuta ‘day care’ moja wanatumia mtaala wa Afrika Kusini hii si sawa ndio maana Serikali tumeandaa kiongozi cha mlezi kitakachoainisha nini motto afanyiwe, afundishwe anapokuwa katika kituo husika.

“...Tumefanya hivyo pia kwa shule za awali ipo mitaala kwaajili ya walimu,” alisema Makona.

Makona alizindua katiba ya Umoja wa Vituo vya kulelea watoto wadogo mchana jijini Dar es Salaam (Uviwada) na kusema idadi ya vituo hivyo Tanzania nzima vipo 6,000 vilivyosajiliwa na nusu yake vipo Dar na kuhimiza mikoa mingine kuanzisha umoja kama huo ili wapate umoja wa kitaifa.

“Tukipata umoja wakitaifa itakuwa rahisi kuwasilishwa changamoto zenu ikiwemo za usajili,” alisema Makona

Mwenyekiti wa Uviwada, Shukuru Mwakasege alisema changamoto nyingine ni watoto ambao wanawafundisha kwa kipindi kinachotakiwa cha miaka miwili hadi minne na miezi 11 kwenda kuanza kuanza shule za awali sehemu nyingine na kukutana na malezi mapya.

“Tunajua hilo ni gumu ila tunaomba mkalifanyie kazi hawa watoto wadogo tuwe nao hadi umri wa kuanza shule ya msingi kabisa,” alisema Mwakasege

Aliongeza kuwa lengo la umoja huo ni kutoa elimu kwa wazazi na wadada kuhusu malezi na makuzi ya mtoto majumbani pia kupata usajili wa vituo vyote Dar chini ya wizara ya ustawi wa jamii.



Naye Mdhibiti Mkuu wa Ubora wa Shule Wilaya ya Temeke, Lilian Kazenga, aliwahimiza viongozi wa UVIWADA kuwahamasisha wamiliki wengine wenye vituo vya kulea watoto kujisajili.



“Ninyi mmetimiza vigezo ndio maana ubora wa malezi kati yenu na wasiosajiliwa ninyi wenyewe mnaona kuna changamoto mno hasa pale walezi wanapotumia mitaala jambo ambalo sio sahihi kwenye vituo kuna miongozo sio mitaala,” alisisitiza Kazenga.

No comments:

Post a Comment

Pages