HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 25, 2022

Wanaonyanyaswa, kupata mimba walindwe kisheria


Na Mwandishi Wetu

KATIKA kuhakikisha waathirika wa unyanyasaji wa kijinsia wanapewa kipaumbele, imebainika kuwa ipo haja ya kurekebisha baadhi ya sheria ili kuokoa maisha ya waathirika hususani wa mimba zisizotarajiwa kutokana na unyanyasaji huo.

Hayo yalibainishwa juzi jioni na Mtaalamu wa masuala ya Afya na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Marie Stopes, Sivaramkrishnan Chandrashekar alipozungumza na waandishi wa habari wakati wa furari iliyoandaliwa na shirika hilo kwa wadau wake.

Futari hiyo iliwakutanisha wadau na wateja wa Shirika l Marie Stopes Tanzania (MST), kutoka taasisi mbalimbali ambazo ni benki, makampuni mbalimbali na

Chandrashekkar alisema pamoja na sheria za Tanzania kuzuia utoaji mimba kuna baadhi ya vifungu katika sheria hiyo vinavyoruhusu utolewaji wa mimba endapo mjamzito yuko hatarini.

“Kwa hiyo si ukweli kusema kwamba Tanzania inapiga marufuku utoaji mimba kwa sababu nchi hii imeingia na kusaini itifaki ya Maputo,” alisema.

Itifaki hiyo imezungumzia masuala ya haki za binadamu kwa wanawake wa Afrika ikiwemo haki na utu wao, haki ya kulinda afya yao ya uzazi na idhini ya kutoa mimba wanaponyanyasika kijinsia na kubakwa.

“Nafikiri kuna haka ya kuziangalia sheriq na sera zinazohusiana na unyanyasaji wa kijinsia ili kuwalinda waathirika wasikimbilie kwenye utoaji mimba usio salama,” alisema.

Aliongeza kuwa ni vyema masuala yanayohusu imani za jamii na mila na desturi nayo yakaangaliwa.

Kwa mujibu wake ni muhimu kwa vijana wa kike waliopo shule za Msingi kupatiwa elimu kuhussu afya ya uzazi kwa kuzingatia umri wao.

Alisema katika dunia ya sasa vijana wana fursa ya kupata taarifa kupitia maeneo mbalimbali ikiwemo mitandao ya kijamii hivyo ni muhimu kwa vijana hao kupata taarifa kupitia vyanzo sahihi.

Alisisitiza kuwa pamoja na vijana hao kupatiwa taarifa ni muhimu kuhakikisha kuwa taarifa hizo zinaendana na umri wao na hali halisi ya mabadiliko ya miili yao.

Alieleza kuwa vijana wa kike wenye umri wa kuanzia miaka nane hadi 10 wanaweza kufundishwa kuhusu usafi wao binafsi hadi watakapofikia umri wa balehe wakiwa sekondari na vyuoni ndio wanaweza kufundishwa kuhusu kujikinga na mimba zisizotarajiwa.

“Wazazi na walimu mara nyingi hawazungumzi na watoto wa kike kuhusu masuala ya afya ya uzazi. Endapo elimu hii utatolewa kwa vijana hawa katika umri sahihi kuna uwezekano wa mabadiliko makubwa katika maisha yao,” alisisitiza.

Aliipongeza serikali kwa kuiunga mkono MST tangu ainze kutoa huduma miaka 32 iliyopita ikilenga masuala ya afya ya uzazi, uzazi wz mpango na utoaji mimba salama hali iliyosaidia shirika hilo kuboresha zaidi huduma zake.

No comments:

Post a Comment

Pages