HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 19, 2022

'WATANZANIA' TUSIPO UHESHIMU MPIRA HAUTATUHESHIMU MILELE


Mchezo wa Soka ni mchezo wenye hisia za tofauti sana na michezo mingine ndio maana hata asiyekuwa na uelewa nao anahaki ya kutoa maoni na akajihishj yuko sahihi kwa sababu macho ya nyama yameona.

Na hapa ndipo matarajio yasipotimia hisia huunajisi Mpira kwa kauli hasi.

Ni wapi tumeona timu inapaswa kucheza dakika 45 pekee na kupata matokeo ya dakika 90 bila kucheza dakika 45 za pili?? Ni sheria ipi inayolazimu timu kushinda kwake tu na kuwa mshindi wa ugenini eti kisa imeshinda kwake mabao mengi??

PSG waliwahi kuifunga FC Barcelona mabao 4-0 Paris lakini walikwenda Camp Now walikufa 6. wakatolewa, Mpira hauchezwi dakika 45 pekee bali 90.

Ushidi wa Simba dhidi ya Orlando Pirates ni ushindi muhimu katika hatua muhimu sana na ngumu kuliko huo ushindi wa kufikirika.

Simba walikuwa na mpango sahihi, Pirates walikuwa na majibu sahihi, Simba wakashindwa kufanya baadhi ya vitu vya ziada kama kuwa na mikimbio mingi nyuma ya mstari wa viungo wazuiaji, mbele ya mabeki wa Orlando. 'between the lines'

Kuanza na Sakho, Morrison na Banda, Pablo alikuwa sahihi na hata substitution alizofanya alikuwa sahihi issue ni jinsi gani wachezaji walilazimishwa kushindwa kuwa na second option kuibeba timu hapo hawakuwa na kosa ni mbnu ziliumana jino kwa jino.

Orlando kuja na mpango wa 4.4.1.1 wakilinda na 4.3.3 wakishambulia, kiulinzi walifanikiwa lakini katika kushambulia walikuwa na vigugumizi vichwani mwao kwa kuihofia Simba. Hivyo ndivyo mechi kubwa huchezwa na Simba walifanikiwa.

Tunaotaka Simba icheze dakika 45 na kuwa mshindi wa dakika 90 labda mchezo mwingine tumeuvumbua ila kama ni ⚽ basi tuuheshimu maana timu kubwa haina nyumbani wala ugenini lazima upambane hasa katika hatua za mechi kubwa kama hizi.

Hapa ndipo tunahitaki kuona ukubwa wa benchi la ufundi la Simba, hapa ndipo Simba inapaswa kuwa na majibu ya Robo Fainali zilzizopita kwa kufanya vizuri ugenini hata kwa kupata sare.
 

NB. Licha ya ubora wa Orlando waliouonyesha jana lakini wakifunguka wakohatarini kuliko wakipaki basi.
It's not over until it is over 🦁
✍️@johmasterplan



No comments:

Post a Comment

Pages