Sisty Nyahoza, Katibu wa Kikosi Kazi cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Na ORPP
Kikosi
Kazi cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kimebadili ratiba yake
iliyotolewa tarehe 5 Mei, 2022. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na
Katibu wa Kikosi Kazi hicho Sisty Nyahoza, wajumbe wa Kikosi Kazi wataanza
kukutana na taasisi pamoja na watu binafsi badala ya vyama vya siasa kama
ilivyoelezwa awali.
Kwa
mujibu wa ratiba hiyo Kikosi Kazi kitaendelea kukutana na wadau mbalimbali wa demokrasia
ya vyama vingi nchini kuanzia siku ya Jumanne tarehe 10 Mei, 2022 kwenye ukumbi
wa Chifu Adam Sapi Mkwawa, ofisi ndogo za Bunge Jijini Dar-es-salaam. Siku hiyo
Kikosi Kazi kitaanza kwa kukutana na taasisi ya The Right Way kuanzia saa nne hadi
saa tano asubuhi. Mchana kuanzia saa sita kitakutana na Msajili wa Vyama vya
Siasa Mstaafu John Tendwa na kukamilisha ratiba yake kwa kukutana na Kituo cha
Utawala Bora na Maendeleo (CEGODETA) kuanzia saa nane hadi tisa mchana.
Siku
ya Jumatano itakuwa zamu ya Jumuiya ya Wahindu Tanzania kuanzia saa nne hadi
tano asubuhi. Mchana Kikosi Kazi kuanzia saa sita mchana kitapata wasaa kupokea
maoni ya Sheikh Ponda Issa Ponda na baadae Askofu Emaus Mwamakula wa Kanisa la
Moravian.
Alhamisi
Kikosi Kazi saa nne asubuhi kitakuna na Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri
Dayosisi ya Karagwe Benson Bagonza, mchana kuanzia saa sita itakuwa zamu ya Dkt.
Hellen Kijo Bisimba kuwasilisha maoni yake na baadae kitapokea maoni ya mwanazuoni
wa fani ya sheria Profesa Issa Shivji.
Siku
ya Ijumaa Kikosi Kazi kitapokea maoni ya mwanasheria na mwanahabari mkongwe
Jenerali Twaha Ulimwengu na mwanasheria Fatma Karume kuanzia saa tatu hadi tano
asubuhi.
Ratiba
ya inaonesha wiki inayoanza tarehe 16 Mei, 2022 Kikosi Kazi kitaendelea kukutana
na taasisi mbalimbali na watu binafsi. Kikosi Kazi kitakutana na taasisi kama
Chama cha Wakulima Tanzania (TASO), Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora,
Mtandao wa Wanawake wa Katiba, Uchaguzi na Uongozi Tanzania. Watu binafsi ni pamoja
na mwanahabari Maria Sarungi, Wadhibiti na Wakaguzi Wakuu wa Hesabu za Serikali
wastaafu Profesa Mussa Assad na Ludovick Utouh.
No comments:
Post a Comment