Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Toma Mtume - Muungano, George Sai, (kulia) akilishwa keki wakati wa uzinduzi wa Jubilei ya miaka 50 ya WAWATA iliyofanyika kanisani hapo jijini Dar es Salaam.
Mashangwena wakifungua fataki za maua kusherekea miaka 50 ya WAWATA.
Uzinduzi wa huo ulianza na ibada ya Misa takatifu ya miaka 50 ya WAWATA iliyoongozwa na Paroko wa Parokia ya Mtakatifu - Toma Mtume Muungamo Padri George Sai akisaidiwa na Padri Gabriel Kpohihin
Akiendesha ibada hiyo ya Shukrani BabavParoko Sai aliwataka Wanawake Wakatoliki wa Parokia hiyo walio na umri wa miaka 35 na kuendelea kujiunga na kulitumikia kanisa Kwa Upendo bila kuchoka ,kama Kauli mbiu ya WAWATA inayosema "Kwa Upendo wa Kristo Tumtumikie na Kuwajibika."
Chama cha kitume cha Wanawake Wakatoliki Tanzania(WAWATA) kilianzishwa mwaka 1972 na mwaka huu kinatimiza miaka 50
Katika uzinduzi huo Wanawake hao walifundishwa mambo mbalimbali ikiwemo mada ya Afya ya Akili iliyowasilishwa na Dkt. Esther Stephen kutoka Chuo Kikuu cha Afya na Sanyansi Shirikishi cha Muhimbili na Bi zitta Mnyanyi aliyewasilisha mada kuhusu Wito na Dhamana ya Wanamke katika Maisha na Utume wa Kanisa
No comments:
Post a Comment