Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka akizungumza wa Baraza hilo la Eidy Wilayani Kibaha.
Na Victor Masangu, Kibaha
Mbunge
wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka ameungana kwa pamoja na
waamini wa dini ya kiislamu katika Baraza la sikukuu ya Eid ambapo
ameahidi kuchangia mifuko 100 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa ofisi ya
Bakwata Wilaya ya Kibaha.
Koka
ametoa kauli hiyo wakati wa sherehe za Baraza hilo ambalo limefanyika
katika shule ya msingi iliyopo kata ya Visiga Wilayani Kibaha Mkoa wa
Pwani ambapo limehudhuliwa na viongozi mbali mbali wa dini na serikali.
Alisema
kwamba ofisi yake imekuwa bega kwa bega katika kushirikiana na Bakwata
Wilaya tangu mwaka 2017 katika kuandaa Mabaraza hayo ya Eid lengo ikiwa
ni kuweza kukutana kwa pamoja baada ya kumalizika kwa mfungo wa mwezi
mtukufu wa Ramadhani.
"Mimi ofisi yangu imekuwa mstari wa mbele katika kuboresha mahusiano
mazuri na wenzetu wa Bakwata bila kujali itikadi zozote za kidini kwa
hivyo nimeamua kuchangia mifuko 100 ya saruji ambayo nina Imani itaweza
kuleta mwanzo mzuri katika kuanza ujenzi,"alisema Koka
Aidha ameongeza kuwa pamoja na Mambo mengine ataendelea kushirikiana na
viongozi mbali mbali wa dini katika kuchochea zaidi kasi ya maendeleo
kwa wananchi wa Jimbo lake la Kibaha mji ikiwemo miundombinu ya barabara
maji,umeme,afya pamoja na Mambo mengine.
"Nampongeza
Sana Rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan kwa kuweza kuleta mabadiliko
chanya ya kimaendeleo tangu aingie madaraka ameweza kutoa fedha nyingine
ambazo zimesaidia ujenzi wa vyumba vya madarasa,zahanati,vituo vya afya
pamoja na Mambo mengine mbali mbali,"alisema
Kwa
upande wake Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Pwani Hamis Mtupa aliwataka waamini
wa kiislamu kutumia fursa mbali mbali walizonazo katika kuwasaidia watu
wenye mahitaji wakiwemo wajane pamoja na watoto yatima.
Sheikh
Mtupa aliongeza kuwa waislamu wanatakiwa kuwa wakarimu katika kipindi
chote na sio mpaka uje mfungo wa mwenzi mtukufu wa Ramadhani na
wanapaswa kuwa upendo ili kupata baraka kwa mwenyezi Mungu.
Pia
alimpongeza Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini kwa upendo na moyo wake wa
kujitolea katika kushirikiana katika Mambo mbali mbali ya kimaendeleo
pamoja na kuungana na waislamu katika mambo mbali mbali.
Katika
hatua nyingine aliziomba kamati za ulinzi na usalama kuendelea kuweka
ulinzi madhubuti ili kudumisha hali ya ulinzi na usalama na kuepuka vita
na machafuko Kama nchi nyingine.
Naye
Sheikh wa Wilaya ya Kibaha Said Mtunda alitumia fursa hiyo kimshukuru
Mbunge kwa mchango wake na kuwataka waislamu kuepuka kabisa na vitendo
vya kufanya fujo na badala yake wajikite zaidi katika kutenda Mambo
mema.
No comments:
Post a Comment