Mkurugenzi wa Mamlaka ya Bandari Mkoa wa Dar es Salaam Mhandisi Juma Javara akijibu maswali yaliyoulizwa na Wafanyabiashara katika Kikao cha Mkuu wa Mkoa huo cha kusikiliza kero za wafanyabiashara.
Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam
Mkurugenzi
wa Mamlaka ya Bandari ya Dar es Salaam (TPA) Mhandisi Juma Javara
amewaondoa shaka wafanyabiashara wanaotumia bandari hiyo kwa
kuwahakikishia kuwa sasa hakuna ucheleweshaji wa kutoa makontena ya
mizigo bandarini hapo.
Kauli hiyo ameitoa
jijini Dar es Salaam wakati akijibu maswali kutoka Jumuiya ya
Wafanyabiashara wa jijini humo katika Kikao cha Mkuu wa Mkoa wa Dar es
Salaam cha kusikiliza kero za Wafanyabiashara kilichokutanisha Wakuu wa
Wilaya, Wakurugenzi wa Manispaa, Taasisi ya Sekta Binafsi Nchini (TPSF),
Uhamiaji, Mameneja wa Mamlaka ya Mapato nchini (TRA), Kamati ya Ulinzi
na Usalama ya Mkoa, Maafisa wa TPA na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na
Rushwa (TAKUKURU).
Amesema kuwa kutokana na
maboresho yaliyofanyika bandarini hakuna meli za mizigo zinazokaa muda
mrefu zikisubiri kushusha mizigo iliyo kwenye makontena na bidhaa
nyingine katika bandari hiyo.
" Niwaondoe shaka
wafanyabiashara sasa hivi meli za kontena hazikai zaidi ya siku 7
bandarini mizigo inatolewa kwa haraka sababau ya maboresho
yaliyofanyika," amesema Mhandisi Javara.
Amebainisha
kuwa Rais Samia Suluhu Hassan alitoa Sh Bilioni 12 kwa ajili ya
maboresho na ununuzi wa vifaa ambapo kwa kiasi kikubwa zimepunguza
malalamiko ya ucheleweshaji wa kutoa mizigo bandarini.
Kwa
upande wake, Mkuu wa Mkoa huo, RC Makalla amesema majibu yote
yaliyotolewa na TPA, TRA Uhamiaji na mamlaka nyingine yatawekwa kwenye
maandishi na nakala itapelekwa katika jumuiya hiyo.
Pia
RC Makalla amesema Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam, Hassan Rugwa
ataongoza kamati hiyo itakayojumuisha watu wa TPA, TRA, Uhamiaji, Ofisi
ya Rais na mamlaka nyingine ambapo itakuwa na jukumu la kukutana na
wafanyabiashara kujadili mambo mbalimbali.
No comments:
Post a Comment