Mganga Mkuu wa Serikali, Dkt. Aifelo Sichalwe akizungumza katika Hafla ya Uzinduzi wa Maabara ya Utafiti wa Vinasaba vya Ugonjwa iliyofanyika katika Ofisi za NIMR, jijini Dar es Salaam.
Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam
Serikali
kupitia Taasisi yake ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR)imesema
itahakikisha inaongeza jitihada za kutokomeza Ugonjwa hatari wa Malaria
ambao umendelea kuwa tishio na kusababisha vifo vingi.
Hayo
yamesemwa Jijini humo wakati wa Hafla ya Uzinduzi wa Maabara ya
Kufuatilia Vinasaba vya Ugonjwa wa Malaria na Mganga Mkuu wa Serikali,
Dkt.Aifello Sichalwe amesema kwamba Maabara hiyo ni moja ya mkakati wa
Wizara ya Afya kupitia Mpango wa kudhibiti Malaria Kwa kushirikiana na
Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa( TAMISEMI).
Amebainisha
kwamba Mradi huo wa Maabara ya Ufuatiliaji wa Vinasaba vya Malaria una
lengo la kupata ushahidi wa kina juu ya chanzo kinachosababisha ugonjwa
wa Malaria na kwamba utasaidia wataalamu wa masuala ya tafiti kupata
suluhisho la Kukabiliana na ugonjwa wa Malaria.
"Utafiti
huu wa Vinasaba vya Malaria niwa awamu ya kwanza kutekelezwa hapa
Nchini ,na unafadhiliwa na wadau wetu wa maendeleo ikiwemo Umoja wa
Ulaya(UN) na tunawaomba waendelee kufadhili ,pia tunaendelea kufanya
mazungumzo na wadau wengine waweze kufadhili ile uwe endelevu nakufikia
lengo tulilokusudia" amesema Dkt .Sichalwe.
Dkt.Sichalwe
amefafanua kuwa utafiti huo utasaidia kuwajengea uwezo NIMR Kwa
kuzalisha takwimu za Vinasaba vya Malaria hapa nchini nakuzichakata
Kisha wizara ya Afya itazitumia kufanya maamuzi ikiwemo kuandaa
miongozo,kutunga sera nakutekeleza mikakati mbalimbali ya kupambana na
Malaria huku wakiwa na ushahidi wa kisayansi
Kwa
upande wake, Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Taasisi ya Utafiti wa
Magonjwa ya Binadamu( NIMR) Dkt.Khadij Malima amesema kwamba utafiti wa
Vinasaba vya Ugonjwa wa Malaria umeanza tangu Mwezi Mei 2020 na
utakamilika Mwezi Oktoba 2023 ambapo Kwa sasa umetekelezwa katika Mikoa
kumi na tatu Nchini kote.
Ameitaja Mikoa hiyo kuwa ni Dar es salaam, Morogoro,Dodoma,Manyara,Pwani, Songwe,Ruvuma,Tabora,Tanga, Kagera,Mtwara,Kigoma,Mara.
nakusema kwamba wasimamizi Wakuu wa utafiti huo wa Vinasaba vya Malaria ni Waganga Wakuu wa Mikoa pamoja na Maafisa afya.
No comments:
Post a Comment