HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

May 03, 2022

PROF.MKENDA: KUNA MAGEUZI MAKUBWA MITAALA YA ELIMU INAKUJA

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prifesa. Adolf Mkenda (kulia), akielezea jambo baada ya kupata maelekezo ya Mradi wa Chuo cha Ufundi Dodoma (DTC) kutoka kwa Mhandisi Mkazi Aliki Nziku.

 

Na Asha Mwakyonde, Dodoma

WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa. Adolf  Mkenda amesema kuwa Kuna mageuzi makubwa ya mitaala inakuja hapa nchini ambayo wanaifanyia mapitio ya Sera ya Elimu ya mafunzo ya mwaka 2014.

Hayo ameyasema leo Mei 2,2022,  jijini Dodoma alipofanya ziara ya kukagua ujenzi  wa Mradi wa chuo cha Ufundi Dodoma (DTC),kilichopo Nala, Prof.  Mkenda amesema kuwa maelekezo yaliyotolewa na Rais Samia Suluhu Hassan kwamba watakapo kamilisha mapitio na kuanza kutoa elimu kwa mitaala mipya ambayo yataeleza sera inayopitiwa kuhakikisha wanaongeza ufundi na ujuzi ili wanaomaliza shule waweze kuajiriwa na kujiarika mapema watakapomaliza.

Amesema kuwa kazi hiyo ya kupitia sera na kubadilisha mitaala na kwamba kwa kazi inavyokwenda mwezi Disemba watakuwa na rasmu ambayo itasubiri maamuzi ya serikali.

"Tutakuwa tumefanya mageuzi makubwa hapa nchini ya elimu tangu mwaka 1967 lakini mageuzi haya yatahitaji miundombinu,vifaa na taaluma hii ni sehemu muhimu Sana ya kutupeleka katika mageuzi hayo,"amesema Wazri huyo.

Amesema kuwa watakapokalimisha mradi wa ujenzi wa chuo hicho  utakapo kamilika utakuwa umegharimu kiasi cha shilingi bilioni 100 na utachukua wanafunzi 3000 na VETA zote zitakapoanza kufanya kazi na kwamba hapa nchini kuna jumla ya vyuo vya ufundi 831.

Pia Prof. Mkenda ameongeza kuwa hapa nchini kuna vyuo vya Ufundi vinavyofanya kazi 43 vya serikali na kwamba katika msukumo mkubwa wa serikali ya awamu ya sita chini ya Rais  Samia  wanatarajia mwisho wa mwaka huu kuweza kuwa na jumla  ya vyuo  77.

Amefafanua kuwa  ujuenzi wake utakuwa umekamilika  wa majengo mapya na pia watakuwa na vyuo 23 vinne vya mikoa  na vingine vinamilikiwa na Halmashauri  hivyo  majengo yake yatakuwa tayari na Wizara hiyo  itahakikisha inaweka vifaa pamoja na wakufunzi wa kutosha.

"Hiki ni chuo kikubwa cha Ufundi kwa hatua hii ni cha nne hapa nchini na kitachukua wanafunzi wangi kitakapokamilika kabisa kitachukua wanafunzi 3000 na kwa awamu hii kitakapokamilika kitachukua wanafunzi 1500 kwa awamu hii ya unjenzi tunaouona hapa ambao umegharimu kiasi cha shilingi bilioni 17.9," amesema Prof. Mkenda.

" Utekelezaji wa Mradi huo  hadi sasa umefikia wastani wa asilimia 50 na tayari  na Mkandarasi ameshalipwa kiasi cha zaidi ya shilingi bilioni 6," amesema waziri Mkenda.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Ufundi kutoka Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia Dk.Noel Mbonde,amesema chuo hicho kitakapokamilika kimepanga kutoa kipaumbele kwa fani za Nishati,  kwa upande wa afya kuwa na fani ya Vifaa Tiba na Ujenzi.

"Kwa awamu hii kama vyuo vyetu tunavyo vijenga vikikamilika tutaongeza idadi ya vijana wenye ujuzi zaidi ya asilimia 30," amesema Mkurugenzi huyo.

Awali akiwasilisha ripoti ya mradi huo kwa Prof.Mkenda,Mhandisi Mkazi Aliki Nziku  amessma kuwa  utekelezaji wa (DTC), upo katika awamu ya kwanza inayojumisha ujenzi wa jengo la utawala,bwalo la chakula, majengo mawili ya vitivo ( Departmental buildings), majengo ya madarasa yenye vyumba sita, karakana tatu za mafunzo kwa vitendo.

Mhandisi huyo pia  ameongeza kuwa pia ujenzi huo umejumuisha mabweni mawili ya gorofa tatu Kila moja lina uwezo wa kuchukua wanafunzi 300, nyumba za Watumishi nne na Zahanati.

"Awamu hii ya kwanza ikikamilika itachukua wanafunazi 1500 na mradi mzima utakapo kamilika  utachukua wanafunzi 3000," amesema Mhandisi Nziku.

Mhandisi huyo ameeleza kuwa mradi huo unatekelezwa na Mkandarasi CRJ (EA), ltd kwa gharama ya shilingi bilioni 17.9 na kwamba kwa niaba ya wizara hiyo mradi unasimamiwa na washauri waandamizi kutoka chuo kikuu cha Dar es Salaam Bureau of Industrial Cooperation (BICO), wakishirikiana na washauri waandamizi kutoka Arqes Africa na Build Consul.

"Tunaomba Wizara kuendelea kutupatia ushirikiano zaidi ili kukamilisha mradi wetu kwa wakati  kama ulivyokusudiwa  pia tunaomba hatua zaidi kufuatilia suala la umeme na maji kufika kwenye mradi  kwa wakati," amesema.
 

No comments:

Post a Comment

Pages