HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

May 02, 2022

WANAFUNZI WA MASOMO YA UFUNDI KUNUFAIKA NA MIKOPO IFIKAPO 2023/2024

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Adolf Mkenda, akimkabidhi vitendea kazi Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu(HESLB),Prof. Hamisi Dihenga lleo April 30,2022 jijini Dodoma.


Na Asha Mwakyonde, Dodoma

WAZIRI wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Prof. Aldof Mkenda ameita Bodi ya Elimu ya Juu (HESLB), kujipanga ifikapo mwaka wa fedha 2023/ 2024  ili ianze kutoa mikopo kwa wanafunzi watakaosoma masomo ya Ufundi na Ujenzi kwa nganzi ya Diploma katika vyuo vya Ufundi  lengo likiwa ni kupanua  wigo wa ajira kwa vijana wenye nia ya kusoma masomo hayo.

Pia Waziri Mkenda ameeleza kuwa  Wizara hiyo imetenga fedha katika bajeti ya  2022/2023 kwa ajili ya ufadhili wa elimu ya juu  (scholarships),
kwa wafanafunzi watakaofanya vizuri katika  masomo ya Sayansi ambapo watapata ufadhili huo wa asilimia 100 kwenda kusoma nje ya nchi.

Prof. Mkenda  ameyasema hayo jana Aprili 30,2022 jijini Dodoma wakati akizungumza na Bodi ya Wakurugenzi wa Bodi ya HESLB, amesema kuwa vijana hao watakuwa na ari ya kusoma lakini ndio watakaoweza kurejesha mikopo yao kwa wakati kwa kuwa wataingia katika ajira za moja kwa moja kwa kujiajiri wenyewe.

Amesema kuwa suala la ajira kwa sasa limekuwa ni changamoto kwa vijana ambao wanamaliza vyuo lakini wakisoma masoma ya Ufundi  katika vyuo vinavyosababisha  na serikali ni rahisi wao kujiajiri bila kusubiri ajira serikalini watakapomaliza.

Waziri Mkenda alivitaja baadhi ya  vyuo hivyo vinavyotambulika kuwa ni Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT),Arusha Technical na kwamba wamekubaliana ifikapo mwaka mpya wa fedha 2023/2024  kupeleka fedha kwa ajili ya wanafunazi hao.

Amefafanua kuwa lengo la kutoa taarifa hiyo mapema ni kuwapa nafasi wanafunzi watakaotaka kuomba  kusoma watambue  fursa ya kupata mikopo katika masomo ya Ufundi.

Akizungmzia  ufadhili huo amesema lengo la Serikali ni kuongeza fursa za upatikanaji wa elimu ya juu na kuhamasisha watoto wengi kupenda kusoma masomo ya Sayansi.

" Namshukuru Samia Suluhu Hassan kwa  kuongeza bajeti ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu kutoka bilioni 464 hadi kufikia bilioni 570, kuondoa adhabu ya asilimia 10 ya wanaochelewa kurejesha mikopo na kufuta asilimia 6 ya kulinda thamani," amesema.

Waziri huyo ameongeza kuwa mkopo huo utatolewa kulinaga na taarifa anazozitoa muombaji na kwamba akitoa zisizo za ukweli kutakuwa na changamoto hivyo bodi itaendelea kuchakata zilizo za kweli ili wanaostahili waweze kupata mkopo huo.

Aidha Waziri Mkenda ametoa wito kwa wanafunzi wanaoomba mikopo ya elimu juu kutoa taarifa zote zinazotakiwa kwa ukamilifu na kwa wakati ili waweze kupata mikopo hiyo bila changamoto.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Eliamani Sedoyeka amesema kwa sasa Wizara imejipanga kuhakikisha Watanzania wengi wanapata fursa ya kusoma elimu ya juu kwa kuwezesha kufanya hivyo kulingana na malengo ya Taifa letu.

“Wote tunafahamu juhudi ambazo Serikali imeweka kwenye elimu msingi ambazo zimepelekea kuwa na idadi kubwa ya wanafunzi wanaomaliza kidato cha nne na sita na wakiwa na ubora na kupelekea kuwa na vigezo vya kuendelea na elimu katika ngazi inayofuata hivyo kupekelea kuhitajika fedha kwa ajili ya kusomesha,” amesema Prof. Sedoyeka.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB),Prof. Hamisi Dihenga amesema anatambua kuwa wana dhamana kubwa ya kuhakikisha utaratibu wa kutoa mikopo unaeleweka kwa Watanzania wote na unawasaidia wale wanaostahili kupata mikopo.

No comments:

Post a Comment

Pages