Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam
Naibu
Waziri huyo ametoa agizo hilo leo Dar es salaam katika kikao kazi
kilichohusisha wajumbe kutoka sekta mbalimbali ikiwemo Wizara
hiyo,mara baada ya kujadili malalamiko yaliyowasilishwa na vyama vya
wafanyakazi madereva na Wamiliki wa Vyombo vya Usafiri.
Aidha
amesema kwamba baada ya kupokea malalamiko hayo kutoka vyama vya
wafanyakazi madera serikali imefanya ufuatiliaji nakubaini Jumla ya
Makampuni 73 hayajazingatia takwa la kisheria la kuwataka wamiliki
kuwapa mikataba wafanyakazi wao.
Amebainisha
kuwa Serikali pia imeweka utaratibu Kwa wamiliki wa magari
yanayosafirisha mafuta na gesi nje ya nchi ikiwemo Nchi ya Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Watu wa Kongo kuwalipa posho kwa kuzingatia utaratibu wa
kisheria wa malipo ya siku 20 za kusubiria kushusha na kupakia mzigo
kwa dola 10 za kimarekani Kwa siku sawa na shilingi za kitanzania elfu
23000.
"Serikali
kwa kuzingatia umuhimu wa posho hizi kwa madereva imeshirikisha vyombo
vya utatu vinavyohusika kisheria kuishauri Serikali katika suala hili
ambavyo ni LESCO na Bodi ya Kima cha Chini cha Mshabara kwa sekta
Binafsi na kupokea maoni yao,Maoni hayo ambayo nimeyaridhia ni kiwango
cha malipo ya safari ya kwenda na kurudi na mzigo(retuns )kuwa shilingi
330,000 na malipo ya kushusha na kupakua mzigo kuwa dola 170 za
kimarekani" amesema Katambi.
Nakuongeza
kuwa "Nasisitiza viwango hivi vya posho ni sehemu ya mkataba wa hali
bora kwa Wafanyakazi Madereva ambavyo vitapaswa kuzingatiwa na waajiri
katika Mikataba ya ajira za Madereva.
Pia
amesema kuwa serikali itaendelea kufanya kaguzi za kazi ikiwa ni pamoja
na kukagua mikataba hiyo kama imezingatia Makubaliano hayo,nakwamba
kuhusu utaratibu wa kupakia na kushusha mafuta na gesi, Serikali imetoa
Mwongozo wa kupakia na kushusha mafuta wa mwaka 2021 kwa wadau wote wa
usafirishaji wa mafuta.
"Ni
jukumu la kila Mdau kuhakikisha taratibu za upakiaji mafuta zinafuatwa
wakati akiwa katika bohari yoyote,serikali itaendelea kutoa elimu kwa
wadau wote ili waweze kuzingatia Mwongozo huu na hatua za kisheria
zitachukuliwa kwa wadau watakaokiuka." Amesema Katambi.
No comments:
Post a Comment