Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dk.
Francis Michael (kushoto), akipata maelezo alipotembelea banda la Tume ya Vyuo Vikuu
Tanzania (TCU) wakati wa kilele cha Maonesho ya 17 ya
Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
SERIKALI
inaendelea na programu mbalimbali za maboresho ya elimu ya vyuo vikuu
nchini, ambapo katika mwaka huu wa fedha zaidi ya mitaala 300 inafanyiwa
mapitio na kuhuishwa kwa kuzingatia maoni ya wadau mbalimbali ili
kukidhi matarajio yao na mahitaji ya soko.
Ameyasema
hayo leo Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt.
Francis Michael wakati akifunga Maonesho ya 17 ya
Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini
Dar es Salaam.
Amesema
Wizara kupitia TCU itaendelea kutoa mafunzo ya kubadilishana uzoefu kwa
wana taaluma wa vyuo vikuu kuhusiana na mbinu bora za ukusanyaji wa
maoni ya wadau na vigezo vya uandaaji na uhuishaji wa mitaala
itakayozingatia mahitaji ya wadau na soko la ajira.
“Wizara
imesaini dola za kimarekani milioni 625 kwa ajili ya kujenga Vyuo Vikuu
Vishiriki katika Mikoa ambayo isiyokuwa na vyuo vikuu, na Tanzania Bara
na Zanzibar kote watapata vyuo vikuu vishiriki ambavyo baadae
vitatanuka na kuwa vyuo vikuu,” Amesema
Aidha
amesema Serikali imekuwa ikijivunia mafanikio makubwa katika sekta ya
elimu kwa upande wa elimu ya juu imeimarisha mifumo ya udhibiti ubora wa
elimu inayotolewa na vyuo vikuu nchini ili kukidhi viwango vya
kitaifa, kikanda na kimataifa.
Pamoja
na hayo amesema Serikali kwa kushirikiana na TCU inawajibu wa
kuendeleza maonesho hayo kila mwaka hivyo taasisi za vyuo vikuu viongeze
muunganiko na vyuo vya nje ili kuwekeza kwenye elimu.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa Bodi Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) Prof.
Penina Muhando amesema maonesho hayo yana lengo ya kujenga na kuimarisha
mahusiano baina ya taasisi zetu za elimu ya juu .
"Maonesho
haya yatawezesha wananchi kupata fursa za kuona shughuli mbalimbali
zinazotendwa na taasisi za elimu ili kuwasaidia wanaotaka kuendelea na
elimu ya juu kufanya maamuzi ya kujiendeleza". Amesema Prof. Muhando.
Naye,
Makamu Mkuu wa Chuo cha Kilimo Sokoine (SUA), Profesa Raphael Chibunda
akizungumza kwa niaba ya washiriki wote alihimiza uwepo wa maonesho hayo
kila mwaka kwa sababu yamekuwa yakisaidia bidadi ya wadahili
kuongezeka.
No comments:
Post a Comment