Mkurugenzi wa Upendo Media, Neng'ida Johannes.
Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam
Waimbaji
Nyota wa Nyimbo za Injili Rose Mhando na Zaza Mokheti kutoka Afrika
Kusini wanatarajia kutumbuiza katika Tamasha la Twen'zetu kwa Yesu
linalotarajiwa kufanyika Agosti 13 mwaka huu katika Uwanja wa Uhuru
jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na wanahabari
leo jijini humo Mkurugenzi wa Upendo Media, Neng'ida Johannes, amesema
kuwa tamasha hilo limeandaliwa na Kanisa la Kiinjili na Kilutheri
Tanzania (KKKT) na kwamba limelenga kuwajenga vijana kua na maadili
mema.
" Tamasha hili linafanyika kwa mwaka wa
tisa tangu lilipoasisiwa mwaka 2014 katika kipindi hicho tamasha
limekuwa likiwagusa vijana wa aina zote, kwani paoja na kwamba
linaandaliwa na taasisi ya kikanisa lakini hili si kwa ajili ya Wakristo
tu bali wa imani zote," amesema Neng'ida.
Amebainisha
kuwa vijana zaidi ya 25,000 wengi kutoka Dar es Salaam wengine kutoka
mikoa ya jirani pamoja na wa nchi za Rwanda, Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Kongo (DRC) na Uganda.
Amesisitiza kuwa tamasha
hilo limebeba kauli mbiu isemayo Wazamani Siwasasa likihimiwahiza
vijana kuachana na mabo ya kizamani badala yake waishi kisasa kwa kuacha
tabia za uongo, ulevi, fitina, uvivu na mahusiano yasiyo mema.
Ameongeza
kuwa tamasha litaanza saa 2 asubuhi mpaka saa 12 jioni huku viingilio
vitakuwa Sh 5000 na kwamba tiketi zinapatikana Mlimani City, KKKT-
Mbezi, Kimara, Mbagala na Luther House- Upendo Media.
Amesema kuwa Askofu wa KKKT Dayosisi ya Mashariki na Pwani Dkt. Alex Malasusa atafungua tamasha hilo litakuwa
na wanenaji mbalimbali ambao watanogesha tamasha hilo akiwemo Mkuu wa
Mkoa Mstaafu wa Tabora, Agrey Mwanri, Mchungaji Msaidiziwa Dayosisi ya
Mashariki, Deogratius Msanya.
Amewataja
waimbaji na kwaya mbalimbali zitakazotumbuiza katika tamasha hilo ni
Rehema Semfukwe, Hyper Squad, Yamungu Mengi (Komando wa Yesu), Kwaya ya
AIC Chang’ombe, The Survivor Kwaya ya Efatha Morovian, Essence of
Worship, Praise Team ya KKKT, DMP Jimbo la Magharibi, Kwaya ya Vijana
KKKT Usharika wa Vituka, Kwaya ya Uinjilisti Haleluya ya KKKT Usharika
wa Mbezi Beach, Kwaya ya Vijana Mabibo Farasi, Kwaya ya Vijana KKKT
Kitunda Relini na Kwaya ya Vijana KKKT Kinyamwezi.
Amweaondoa
hofu watakaoenda tamshani kwani Jeshi la Polisi Mkoa wa Temeke
limejipanga kuimarisha ulinzi na usalama kwa kushirikiana na vikosi
vingine vya ulinzi.
Kwa
upande, Meneja wa Uwanja huo, Redempta Nyahonge amesema wamejipanga
vyema kiusalama licha ya kuwa na Mechi ya Simba na Yanga itakayochezwa
Saa 1 usiku siku katika Uwanja wa Benjamini Mkapa.
Pia
amesema watu wataingia uwanjani hapo upande wa Mageti makubwa ya uwanja
wa nje na kwamba magari yataegeshwa eneo la uwanaja huo.
No comments:
Post a Comment