Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum Dar es Salaam, ACP Jumanne Muliro.
Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam
Jeshi
la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam limesema halitamvumilia mtu au
kikundi cha watu kitachojihusisha na vitendo vya uvunjivu wa amani
kuelekea Mechi ya Ngao ya Jamii kati ya Simba na Yanga itakayochezwa
Agosti 13 mwaka huu katika Uwanja wa Benjamini Mkapa, jijini Dar es
Salaam.
Akizungumza
na wanahabari leo jijini humo Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum Dar es
Salaam, ACP Jumanne Muliro amesema jeshi hilo limejipanga vyema
kuhakikisha kabla na baada ya mechi hali ya usalama na amani inatawala
uwanjani hapo hivyo atakayebainika kwenda kinyume watamchukulia hatua za
kisheria.
‘Usalama
utaimarishwa kwa kiwango cha juu. Ni marufuku kwa mtu yeyote kwenda na
silaha uwanjani isipokuwa vyombo vya dola vyenye jukumu la usalama eneo
hilo. Tunawatoa hofu mashabiki watakaofika kushuhudia mchezo huo kuwa
ulinzi ndani na nje ya uwanja utakuwa umeimarishwa kwa kiwango cha
juu’amesema Kamanda Muliro.
Amesisitiza
kuwa wamepiga marufuku kikundi au mtu yeyote kwenda na silaha
uwanjani isipokuwa vyombo vya dola vyenye jukumu la usalama eneo hilo
hivyo atayekiuka hawatasita kumchukulia hatua.
Ameongeza
kuwa kuwa hali ya usalama kwa Jiji la Dar es Salaam inazidi kuimarika
kutokana na wananchi kuendelea kutoa taarifa mbalimbali za
wahalifu,hivyo Polisi wamekuwa wakizingatia maadili, weledi na kuzitunza
siri za wananchi.
Amewaomba
wananchi kuendelea kuimarisha mifumo ya ulinzi shirikishi ikiwa ni
pamoja na kutekeleza falsafa ya ulinzi shirikishii li kuzuia vitendo vya
kihalifu.
Pia
amesema jeshi hilo linaendelea na operasheni maalum kali ya kuzuia
vitendo vya kihalifu maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam.
No comments:
Post a Comment