Mkurugenzi wa Taasisi ya Fikra Afya, Shabil Hussein Khalfan akiwa katika banda la taasisi hiyo kwenye Kambi ya Huduma na Matibabu iliyotolewa na Jumuiya ya Madhehebu ya Khoja Shia Ithasheria kwenye viwanja hivyo.
Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam
Jamii
imeshauriwa kuacha tabia kuwanyanyapaa watu wenye matatizo ya afya ya
akili badala ijenge utamaduni wa kukaa nao karibu kwani wanaweza
kupatiwa matibabu wakaishi maisha ya kawaida.
Hayo
yamesemwa jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Taasisi isiyo ya
Kiserikali ya Fikra Afya inayojishughulisha na Kupambana na Unyanyapaa
uliopo kuhusu Magonjwa ya Akili na Kuelimisha Umma kuhusu Afya ya Akili ,
Shabil Hussein Khalfan kwenye Kambi ya Huduma za Afya na Matibabu
zilizotolewa na Jumuiya ya Madhehebu ya Khoja Shia Ithnasheri kwenye
Viwanja vya Mnazi Mmoja.
Amesema kuwa jamii
ianatakiwa kutambua umuhimu wa afya ya akili sawa na ya afya ya
kiwiliwili hivyo lazima ijenge tabia ya kujilinda na afya hiyo sio tu ya
kiwiliwili pamoja na unyanyapaa kwa wagonjwa wa akili kwani matibabu
yapo na wanaweza kuishi maisha ya kawaida.
"
Tunajaribu kuilemisha jamii kuwa afya ya akili ni muhimu sawa na afya
ya kiwiliwili sio tu kiwiliwili lazima tuwe na tabia ya kujilinda sio tu
ya kiwiliwili na tupambane na unyanyapaa wa watu wenye magonja ya akili
sio kwamba walijiamulia matibabu yapo na wanaweza wakaishi maisha ya
kawaida," amesema Shabil.
Amebainisha kuwa
wameamua kutoa huduma mbalimbali kusaidia ubinadamu kwa kuenzi mafunzo
ya mhenga wao Imam Hussein aliyefanyiwa ukatili huko Kerbal katika karne
ya 61.
Amesisitiza kuwa Imam Hussein alisimama
mbele ya watu waliotaka kumkandamiza na kusimama kwa kusema lazima haki
ieleweke kwa kuwajali, kuwaheshimu na kuwathamini binadamu na kila mtu
ana haki ya kuishi huru ili aweze kujiendeleza.
Ameongeza
kuwa watu waliofika kwenye kambi ya macho, kisukari, afya ya akili,
presha walipatiwa huduma za vipimo na matibabu na kwamba kulikuwa na
kambi ya kukusanya damu kwa kushirikiana na Mpango wa Taifa wa Damu
Salama.
Amefafanua kuwa kwenye kambi hizo
kulikuwa na shule kwa jina la Imam Hussein iliendeshwa kwa watu
waliofika viwanjani hapo ambapo walipatiwa mafunzo na maadili
aliyoyasimamia
No comments:
Post a Comment