HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 24, 2022

MAMBOSASA AWAASA ASKARI POLISI WANAOHUDUMIA MADAWATI YA USALAMA KWANZA KULETA TIJA JESHINI

Mkuu wa Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam Kamishna Mwandamizi wa Polisi Lazaro Mambosasa amewataka Askari Polisi wanaohudumia madawati ya Usalama Kwanza kutumia mafunzo waliyoyapata kuleta tija ndani ya Jeshi la Polisi.

Alisema hayo alipokutana na askari hao katika mwendelezo wa mafunzo ya siku saba ya kuwajengea uwezo wa afya ya akili na msaada wa kisaikolojia kwa watoto. 


Mkuu wa Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam Kamishna Mwandamizi wa Polisi Lazaro Mambosasa,  akizungumza na washiriki wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wa afya ya akili na msaada wa kisaikolojia kwa watoto yanayoendelea jijini Dar es Salaam. (Picha na Datus Mahendeka wa Jeshi la Polisi, Dar es Salaam).

No comments:

Post a Comment

Pages