Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam
Msanii
wa Bongo Movie Steve Mengele" Steve Nyerere" amewasihi Watanzania
kuendelea kuchangia kodi kupitia tozo za miamala ya benki na simu kwa
madai kuwa tozo hizo zinasaidia kuleta Maendeleo Kwa Taifa.
Hayo
ameyasema Jijini Dar es salaam wakati akizungumza na wanahabari ambapo
amesema kwamba jambo la tozo lipo duniani kote nakwamba ni Jambo ambalo
la tija kwa Taifa kutokana na kutatua changamoto mbalimbali za Maendeleo
Kwa wananchi.
Aidha
amebainisha kuwa Serikali ya Awamu ya Sita inataka kuwafikisha
watanzania kwenye hatua ya Maendeleo ya kujivunia wenyewe hivyo na
kuondokana na kutegemea hisani kutoka mataifa ya nchi za nje ikiwemo
Ulaya na Asia.
" Tozo
hizi zipo duniani kote,tusiwekeze siasa na Kodi, watanzania wote
tujivunie na tozo zilizopo ,kama tozo hii ina problem( tatizo) kidogo
inaweza kusawazishwa tu na mambo yanaendelea na siyo kuiondoa kabisa"
amesema Steve.
Amesisistiza
kuwa tozo hizo zinasaidia kukamilisha miradi ya kimkakati ikiwemo
kujenga Barabara ,Madaraja,Reli ya Kisasa,Hospitali ,na miradi mingine
ya maendeleo,hivyo watanzania wanapaswa kushikamana na serikali katika
kutekeleza Ujenzi wa miradi hiyo kupitia tozo.
Ameongeza
kuwa endapo Watanzania watekeleza tozo hizo watakuwa wameonyesha
uzalendo wa hali ya juu nakwamba hata nchi zingine zilizoendelea
akitolea mfano China, Singapore,na Malasia zinategemea kodi kutokana na
tozo.
"Kuna wengine
tumewaona wanaenda Mahakamani kupinga tozo hizi,pia kuna wasanii
wanakurupuka kutunga nyimbo za tozo nimezungumza na BASATA isiruhusu
nyimbo hizo za upotoshaji,kwani uhuru tukiuruhusu sana utatugawanya"
amesema.
Hata hivyo ametumia
fursa hiyo kuwaomba Viongozi wa Dini,Wanasiasa,na Waandishi wa habari
kuelimisha Jamii kuhusu umuhimu wa tozo zinazotozwa kwenye miamala ya
kibenki na simu ili kuondoa sintofahamu Kwa wananchi.
No comments:
Post a Comment